Pata taarifa kuu
TANZANIA

Tanzania yatoa tahadhari ya mlipuko wa Homa ya uti wa mgongo

Serikali ya Tanzania imewataka raia wake kuchukua tahadhari kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo uliotokea katika jimbo la Tshopo nchini DRC Congo.

Sehemu ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lililoko mjini Dodoma Tanzania ambako ni makao makuu ya Serikali.
Sehemu ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lililoko mjini Dodoma Tanzania ambako ni makao makuu ya Serikali. Ikulu/Tanzania
Matangazo ya kibiashara

Vimelea vya ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa au kukaa na mtu mwenye maambukizi, kulingana na wataalam wa magonjwa sugu ya maambukizi.

Mlipuko wa Homa ya uti wa mgongo ni tishio kwa sasa barani Afrika, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa Septemba 8, 2021 na Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika.

Taarifa iliyotolewa jana Alhamisi Septemba 16, 2021 na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Aifelo Sichwale, imesema ni vyema kuendelea kuchukua tahadhari kwani magonjwa hayana mipaka, hususani mikoa ya Tanzania inayopakana na DRC, ikiwemo Kigoma, Rukwa, Kagera, Katavi na Songwe.

.“Ugonjwa huu huchukua siku mbili hadi 10 tangu kuambukizwa hadi kuanza kuonyesha dalili,” amesema Dk  Sichwale.

Kulingana na BBC Mganga mkuu wa serikali ya Tanzania Dkt. Aifelo Sichwale amesema kuwa Wizara inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa ugonjwa huo nchini DRC na kuchukua hatua ili kuzuia na kujiandaa kukabiliana na tishio la ugonjwa huo endapo utajitokeza nchini kama alivyozungumza na Martha Saranga

Dalili

Wataalam anasema dalili kuu za ugonjwa huu ni pamoja na homa kali, kichwa kuuma, kutapika, kuogopa mwanga, kuchanganyikiwa na shingo kukakamaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.