Pata taarifa kuu

Tanzania yawataka raia wake kuwa makini na magonjwa ya kuambukiza

Nchini Tanzania, Wizara ya afya, imewataka raia wake kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya kuambukiza, wakati huu hospitali nyingi nchini humo, zikiripoti ongezeko la wagonjwa wanaougua mafua, kifua na maumivu ya viungo.

Moja ya mitaa ya Dar es Salaam. Baadhi ya raia kupitia mitandao ya kijamii wamedai kusumbuliwa na mafua makali, hali ambayo imeibua hofu kuwa huenda ni maambukizi ya virusi vya Corona.
Moja ya mitaa ya Dar es Salaam. Baadhi ya raia kupitia mitandao ya kijamii wamedai kusumbuliwa na mafua makali, hali ambayo imeibua hofu kuwa huenda ni maambukizi ya virusi vya Corona. © Guy Tillim, Courtesy of Stevenson, Cape Town and Johannesburg
Matangazo ya kibiashara

Katibu mkuu wa wizara ya afya nchini humo, Profesa Abel Makubi, amesema wanafuatilia muenendo wa kusambaa kwa mafua na homa na itaendelea kutoa taarifa mara kwa mara.

Kauli yake imekuja wakati huu baadhi ya hospitali zikiripoti kupokea idadi kubwa ya watu wenye mafua, homa na maumivu ya mwili, wataalamu wakisema huenda inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayoshuhudiwa nchini humo.

 Baadhi ya raia kupitia mitandao ya kijamii wamedai kusumbuliwa na mafua makali, hali ambayo imeibua hofu kuwa huenda ni maambukizi ya virusi vya Corona, ukizingatia kilichotokea kuanzia mwishoni mwa mwaka jana hadi mwanzoni mwa mwaka huu, ambapo watu kadhaa waliripotiwa kupoteza maisha kutokana na virusi hivyo.

 Hata hivyo hali hii haijaripotiwa pakee nchini Tanzania, ambapo raia nchini Kenya, wametumia mitandao ya kijamii kuhoji kusambaa mafua wakati huu nchi hiyo ikirekodi uwepo wa wagonjwa wa Omicron.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.