Pata taarifa kuu

Amnesty International: Janga limesababisa vizuizi kwa uhuru wa kujieleza

Serikali nyingi ulimwenguni zimetumia fursa ya janga la virusi vya Corona kuweka "vizuizi" kw uhuru wa kujieleza na kuwanyamazisha wakosoaji, shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International limelaani katika ripoti iliyochapishwa Jumanne, Oktoba 19.

Nchini Tanzania, kulingana na Amnesty, serikali ya rais wa zamani John Magufuli, ambayo imekuwa ikidharau athari za ugonjwa wa Corona na kukataa kuchukua hatua kukomesha janga hilo, ilitumia sheria zinazopiga marufuku na kuadhibu "habari za uwongo" kuzuia hasa kazi za vyombo vya habari.
Nchini Tanzania, kulingana na Amnesty, serikali ya rais wa zamani John Magufuli, ambayo imekuwa ikidharau athari za ugonjwa wa Corona na kukataa kuchukua hatua kukomesha janga hilo, ilitumia sheria zinazopiga marufuku na kuadhibu "habari za uwongo" kuzuia hasa kazi za vyombo vya habari. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Ikijumuishwa na wimbi la habari, hatua hizi za ukandamizaji mara nyingi zimezuia idadi ya watu kupata habari kamili juu ya virusi, hali ambayo ilikuwa muhimu kuwawezesha kukabiliana nayo mara tu janga lilipoibuka mapema mwaka wa 2020, Amnesty International imebaini

"Wakati wote wa janga hilo, serikali zilianzisha shambulio lisilokuwa la kawaida juu ya uhuru wa kujieleza," afisa wa Amnesty International Rajat Khosla amesema katika taarifa. "Njia za mawasiliano zililengwa, mitandao ya kijamii ilikaguliwa na vyombo vya habari vilifungwa," ameongeza, na "waandishi wa habari na wataalamu wa afya wamenyamazishwa na kufungwa."

Kwa mujibu wa Amnesty International, ukosefu wa habari uliosababisha hali kzidi kuwa mbaya na kusababisha janga hilo kuwa na guvu zaidi ikizidisha idadi ya janga hilo, na kuua watu milioni tano.

Kazi za vyombo vya habari zilizuiliwa

"Katika nchi kama Misri, kwa mfano, wahudumui wa afya walikamatwa, kufungwa kiholela kwa kuhoji au kulaani usimamizi wa janga hilo na mamlaka ya Misri na kuishia gerezani katika mazingira maumu ya kizuizini, kwa sababu tu ya kufanya kazi yao, amesema Katia Roux, afisa wa shirika la kimataifa la Haki za binadamu la Amnesty International. Kuna mifano mingi, kwa bahati mbaya, kwani kulionekana watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari, wanaharakati wa kisiasa, wahudumu wa afya, walichunguzwa, kunyanyaswa, kushambuliwa, kushtakiwa ... Na matokeo yake, ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, pia ni kuundwa kwa mazingira ya hofu na vitisho. Walilengwa watu hawa, kwa kuwanyamazisha na kutaka kuzuia sauti zingine zisiongee. Na hiyo pia ni moja wapo ya hitimisho la ripoti hii".

Amnesty International pia inataja kesi ya China ambapo uchunguzi zaidi ya 5,000 wa jinai ulifunguliwa mnamo Februari 2020 dhidi ya watu wanaotuhumiwa "kutunga na kukusudia kueneza habari za uwongo na zenye kudhuru" juu ya chimbuko na kiwango cha janga hilo.

Nchini Tanzania, serikali ya Rais wa zamani John Magufuli, ambayo imekuwa ikidharau athari za ugonjwa wa Corona na kukataa kuchukua hatua kukomesha ugonjwa huo, imetumia sheria zinazopiga marufuku na kuadhibu "habari bandia" hasa kuzuia kazi za vyombo vya habari.

Nchini Nicaragua, mamlaka ilipitisha sheria ya kupambana na uhalifu wa kimtandao, ambao unawaruhusu "kuwaadhibu wale wanaokosoa sera za serikali" na "kukandamiza uhuru wa kujieleza".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.