Pata taarifa kuu
TOGO

Covid-19 Togo: Vizuizi vipya vyazua utata

Kuongezwa kwa kipindi cha hali ya dharura ya kiafya kwa kipindi cha mwaka mmoja, kufungwa kwa maeneo ya ibada, baa na mikahawa, au hata kufika katika ofisi za serikali inatakiwa mtu awe amepewa chanjo dhidi ya Covid-19. Vizuizi ambavyo huonekana kama shinikizo la kulazimisha raia wapewe chanjo. Vyama vya kisiasa na maaskofu hawakubaliani na utaratibu huu wa kampeni ya chanjo nchini Togo.

Mwanamke anatembea katika mitaa ya Lomé, Togo, akiwa na amevaa barakoa, moja ya hatua za masharti dhidi ya Covid-19.
Mwanamke anatembea katika mitaa ya Lomé, Togo, akiwa na amevaa barakoa, moja ya hatua za masharti dhidi ya Covid-19. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Tangu Septemba 9, wakati serikali ilipoongeza hatua hizo, ofisi mbalimbali za serikali zimekuwa zikitoa taarifa kwa raia wanaotafuta hoduma kuweza kupewa chanjo au kuonyesha kibali kuwa wameshapokea chanjo dhidi ya Covid-19.

Katika chuo kikuu, Idara ya Masomo ya Taaluma na Mafunzo inawakumbusha wanafunzi kuwa kufika katika maeneo ya mitihani kutatakiwa mtu awe amepewa chanjo au kuonyesha kibali kinachothibitisha kuwa umefanya kipimo cha PCR kayika kipindi kisichozidi saa 72. Mkurugenzi wa polisi ameamua kutumia utaratibu huo kwa maafisa wa polisi au kwa mtu yeyote anaye jielekeza kwenye vituo vya polisi.

Kampeni hii ya chanjo ya kulazimishwa imepokelewa shingo upande kwa raia wa Togo. Jean-Pierre Fabre, kiongozi wa Muungano wa Kitaifa wa Mabadiliko (ANC) amesema: “Ninasema tunapaswa kupata chanjo. Mamlaka ya Togo wanatumia njia isiofaa kutaka kuwalazimisha watu. Zaidi ya yote, hatupaswi kufanya upinzani kwa wito wa kupewa chanjo, jambpo ambalo serikali inafanya kwa sasa. "

Maaskofu wanalaani utaratibu unaotumiwa na serikali kwa kukabiliana na janga la Covid-19. Askofu Benoît Alowonou, Mkuu wa Baraza Kuu la Maaskofu chini Togo anasema: “Hatusemi kwamba kampeni haiendeshwi vizuri. Walakini, tunahitaji uelimishaji ambao utamuwezesha raia kufahamu kinachotakiwa kufanywa kwa kukabiliana na ugonjwa huo. Makanisa pia yamefungwa. Na bado, pia ni mahali pa elimu ambapo waumini wnatolewa wito kujua hali halisi ya kiafya ya wakati huu. "

Kufikia sasa,  9% watu wenye umri wa miaka 18 na zaidi dio wamepokea dozi mbili za chanjo, na 13% ya watu wenye umri huo wamepokea dozi ya kwanza ya chanjo dhidi ya Covid-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.