Faure Gnassingbe kuwania tena uchaguzi wa urais Togo
Rais wa Togo Faure Gnassingbe amethibitisha kuwania tena urais wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi ujao. Huu utakuwa ni muhula wake wanne kuwania wadhifa huo na kuendeleza rekodi ya fanaili yake kuendelea kuwa madaraka.
Imechapishwa:
Wabunge nchini Togo mwezi Mei mwaka uliopita, walibadilisha Katiba na kumruhusu Gnassingbe kuwania tena kwa muhula mwingine kati ya mwaka 2020-2025.
Mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Togo umesababisha mdororo wa kiuchumi, huku baadhi ya maduka yakiendelea kufungwa kutokana na hali mbaya ya kiuchumi. Raia wanaendelea kukabiliwa na hali mbaya ya kimaisha, huku mashirika mbalimbali yakiwataka wanasiasa, hasa serikali kutafutia ufumbuzi mgogoro huo.
Faure Gnassingbe alichaguliwa kwa muhula mwengine mnamo mwaka 2010 na 2015 katika uchaguzi uliozua utata na kususiwa na upinzani, baada ya kumrithi baba yake aliyetawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 38.