Pata taarifa kuu
TOGO-UCHAGUZI-SIASA

Raia wa Togo wawachagua wabunge wapya chini ya ulinzi mkali

Wapiga kura milioni tatu nchini Togo wanashiriki uchaguzi Alhamisi Desemba 20, 2018. Hata hivyo, muungano wa vyama 14 vya upinzani (C14) umetangaza kwamba hautoshiriki katika uchaguzi huo.

Uchaguzi unafanyika chini ya Ulinzi mkali Togo.
Uchaguzi unafanyika chini ya Ulinzi mkali Togo. Yanick Folly / AFP
Matangazo ya kibiashara

yama kumi na viwili na wagombea binafsi 25 wanawania nafasi 91 za wabunge, kwa jumla ya wagombea 850.

Muungano wa vyama 14 vya upinzani (C14) mpaka sasa una wabunge 25, sawa na robo ya viti vinavyohitajika bungeni. Lakini muungano wa vyama 14 vya upinzani unabaini kwamba kura hii ni pigo kwa upande wa mchakato mzima wa uchaguzi, kwa sababu serikali haijaheshimu ahadi zake katika mpangilio mzima uliyowekwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS). Muungano huo unaonyesha hatua za serikali zisizoridhisha na marekebisho ya kitaasisi na kikatiba. Katika hali hiyo, C14 inabaini kwamba uchaguzi hauwezi kuwa huru na wa wazi.

Mapema mwezi Desemba, muungano wa vyama 14 vya upinzani (C14) uliwataka wafuasi wake kuandamana kwa muda wa wiki mbili ili kuomba kusitishwa kwa mchakato wa uchaguzi. Maandamano ya Desemba 8 na 9 yalizimwa, huku vikosi vya usalama vikishtumiwa kuwaua kwa makusudi watu wanne, ikiwa ni pamoja na watatu waliouawa kwa kupigwa risasi, akiwemo mvulana mwenye umri wa miaka 12.

Uchaguzi huu unafanyika chini ya ulinzi mkali.

Uchaguzi unafanyika licha ya mvutano unaoendelea. Ni vigumu kujua iwapo wafuasi wa C14 watashiriki uchaguzi hio au la au wanangia mitaani.

Zoezi la kupiga kura upande wa vikosi vya usalama siku ya Jumanne 18 likfanyika kwa utulivu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.