Pata taarifa kuu
DRC - Afya

DRC: Raia waliokimbia vita wafariki kutokana na njaa

Raia 2 waliokimbia makazi yao kutokana na vita kati ya waasi wa M23 na jeshi la Congo FARDCwilayani Rutshuru na nyiragongo mkoani Kivu Kaskazini , wamefariki kutokana na njaa katika  kambi yaKanyaruchinya kilomita chache kutoka mji wa Goma mashariki mwa DRC.

Wakimbizi wa DRC wakikimbia makaazi yao Novemba 7 Mwaka 2008.
Wakimbizi wa DRC wakikimbia makaazi yao Novemba 7 Mwaka 2008. UNHCR / P. Taggart
Matangazo ya kibiashara

Familia za mama Sabimana Twize na Baba Serefe Zakee katika kambi ya wakimbizi ya Kanyaruchinya wanakiri kuwapoteza wanao waliofariki kutokana na makali ya njaa, na kuongeza kuwa maisha wanayopitia ni magumu, na juhudi zao kuaotaka serikali kuwasaidia zimegonga mwamba, huku wakitoa wito kwa wasamaria wema kuwasaidia.

Hatua chache  Solange Bweza, kutoka familia hiyo pia anakiri kuwa uhaba wa chakula umekuwa sugu katika kambi hiyo, na kwamba wamekosa kupata misaada.

Mashirika ya kiraia Wilayani Nyiragongo kupitia kwa Boshi Ndacho Erick, yamesema yametumia kila mbinu kushawishi serikali kuwasaidia raia walio katika kambi, lakini hilo halijafanyifa huku, akiri kuwa vifo ambavyo vimeripotiwa katika kambi hiyo vimetokana na njaa.

Shirika la OCHA kupitia kwa mkurugezi wake nchini DRC, Joseph Ingaje, limesema shirika hilo limekuwa likitoa misaada, ila akakiri kwamba wanahitaji pesa zaidi kuwasadia waaathiriwa na chakula zaidi pamoja na maji.

Mwezi uliopita zaidi ya raia 2, 700 wakimbia mwawao nchini DRC, kutokana na vita kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa FRDC, mashariki mwa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.