Pata taarifa kuu
DRC - Rwanda - Usalama

DRC/Rwanda : Marais Tshisekedi na Kagame wakutana nchini Angola

Rais wa DRC Felix Tshisekedi na mwanzake wa Rwanda, Paul Kagame, wamekutana kwa mazungumzo mjini Luanda, Angola, ambapo wamekubaliana kufanya kazi pamoja lishughulikia changamoto za kiusalama baina ya nchi zao.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi akiwa na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame huko Rubavu upande wa Rwanda Juni 25 2021
Rais wa DRC Felix Tshisekedi akiwa na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame huko Rubavu upande wa Rwanda Juni 25 2021 © Ikulu ya Kinshasa DRC
Matangazo ya kibiashara

Mkutano baina ya viongozi hawa wawili, umefanyika chini ya uratibu wa rais wa Angola, Joao Laurenco, ambaye pia ni mwenyekiti wa jumuiya nchi za maziwa makuu.

Taarifa za ndani ya mkutano wao zinasema viongozi hawa wamejadiliana kwa kina kuhusu mzozo uliojitokeza hivi karibuni, hasa suala la waasi wa M23 wa wale wa FDLR, ambapo kila mmoja anadai anatoa msaada kwa kundi moja wapo.

Kwa majumaa kadhaa sasa DRC, inaishtumu Rwanda kuwafadhili waasi wa M23 ambao wameibuka tena hivi karibuni na kuanza mashambulizi dhidi ya vikosi vya serikali na kudhibiti baadhi ya miji.

Hata hivyo Rwanda kwa upande wake, imekana madai hayo na badala yake ikiituhumu DRC kwa kushirikiana na FDLR wanaotaka kuipindua serikali ya Kigali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.