Pata taarifa kuu
Rwanda/DRC - Usalama

DRC/Rwanda : Marais Felix Tshisekedi na Paul Kagame kukutana nchini Angola

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame, wanakutana leo jijini Luanda nchini Angola, kwa ajili ya mazungumzo ya kutatua mvutano wa kidiplimasia kati ya nchi hizo jirani.

Marais Paul Kagame wa Rwanda na rais Felix Tshisekedi wa DRC wakiteta kuhusu mahusiano ya kidiplomasia kati ya Nchi zao, Marchi 2021
Marais Paul Kagame wa Rwanda na rais Felix Tshisekedi wa DRC wakiteta kuhusu mahusiano ya kidiplomasia kati ya Nchi zao, Marchi 2021 © Ikulu ya Kinshasa DRC
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya yataongozwa na rais wa Angola Joao Lourenço,  mpatanishi wa mzozo huu ambao umedumu kwa miezi kadhaa sasa, kati ya Kigali na Kinshasa.

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inaishtumu Rwanda kwa kuwaunga waasi wa M 23 ambao wameendelea kukabiliana na wanajeshi wa serikali, Mashariki mwa nchi yake madai ambayo Kigali inakanusha.

Katika mazungumzo haya, rais Tshisekedi atataka uthibitisho kutoka kwa Rwanda iwapo inawaunga mkono waaasi wa M 23, huku Rwanda nayo ikitarajiwa kugusia madai ya jeshi la DRC kushirikiana na waasi wa FDLR na kutekeleza mashambulio katika ardhi yake.

Mbali na  mazungumzo kati ya marais hao, kutakuwa na majadiliano mengine kati ya wajumbe kutoka nchi hizo jirani, DRC ikiongozwa na mkuu wa masuala ya diplomasia Christophe Lutundula na mjumbe maalum Serge Tshibangu huku upande wa Rwanda ukitarajiwa kuwakilishwa na mshauri wa maalum wa masuala ya usalama James Kabarebe.

Uamuzi wa DRC kusitisha ushirikiano wa kiuchumi na kuzuia safarai za Shirika la ndege la Rwandair ni miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.