Pata taarifa kuu
DRC - Usalama

DRC : Mapigano mapya yaripotiwa kati ya M23 na wanajeshi wa serikali

Mapigano mapya kati ya waasi wa M 23 na wanajeshi wa serikali ya DRC, yameripotiwa Wilayani Rutshuru Mashariki mwa nchi hiyo, siku moja tu baada ya viongozi wa DRC na Rwanda kukubaliana nchini Angola kusitisha mvutano ambao umekuwa, ukishuhudiwa kwa wiki kadhaa sasa.

Wanajeshi wa serikali nchini DRC
Wanajeshi wa serikali nchini DRC RFI / Léa-Lisa Westerhoff
Matangazo ya kibiashara

Kundi la M 23 linasema makubaliano hayo hayawahusu na wataendelea na harakati zao.

M 23 linasema iwapo DRC ina nia ya kumaliza mzozo na kundi hilo, ni sharti likihusishwe kwenye mazungumzo ya kutafuta  amani.

Msemaji wa M23 ,Willy Ngoma, amesema makubaliano ya kati rais wa DRC Felix Tshisekedi na Mwenzake wa Rwanda, kutaka kundi hilo liondoke DRC, hayatakelezwa akisisitiza wapiganaji wa M 23 ni raia wa DRC wanaopigania haki za waliowachache.

Christopher Lutundula, Waziri wa Mambo ya nje hata hivyo amesema taifa hilo linasubiri taifa jirani la Rwanda, kutekeleza yale waliokubaliana katika mkutano wa Angola, kuhusu kurejeshwa kwa amani nchini DRC, kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa.

DRC kwa majumaa kadhaa sasa imekuwa ikituhumu Rwanda kwa kuunga mkono uasi wa kundi la M 23, madai ambayo Kigali imekanusha vikali na kudai DRC ndiyo inalenga kuyumbisha usalama wake kupitia kundi la waasi wa FDLR.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.