Pata taarifa kuu
DRC - Usalama

DRC : Waasi wa M23 wakataa kusitisha mapigano

Waasi wa M23, nchini DRC wamesema mazungumzo ya kutafuta amani kati ya rais wa Rwanda, Paul Kagame na mwenzake wa DRC, Felix Tshisekedi,  hayatasitisha vita vinavyoendelea mashariki mwa DRC.

wanachama wa kundi la M23.
wanachama wa kundi la M23. AFP PHOTO/ ISAAC KASAMANI
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Kundi la M23 Willy Ngoma, amesema hataondoka DRC na kwamba wao ni raia wa DRC na hawezi kuondoka DRC.

Ngoma amesema tatizo la utovu wa usalama mashariki mwa DRC ni la Kisiasa na linastahili kusuluhishwa kisiasa.

Kundi hilo la M23 linasema linapigania haki za raia walio wachache nchini DRC, ila serikali ya DRC inawatuhumu kuwa vijibaraka vya Rwanda.

Mazungumzo ya nchini Angola, chini ya uongozi wa rais João Lourenço, yaliafikia kusitisha mvutano kati ya DRC na Rwanda, ambapo DRC imekuwa ikituhumu Rwanda kuunga mkono waasi wa M23, Kigali ikikanusha vikali madai hayo.

Viongozi wa DRC na Rwanda pia waliafikiana  kuunga mkono kuondoka kwa kundi la M23 mashariki mwa DRC bila vikwazo.

Uhusiano kati ya Rwanda na DRC umekuwa tete tangu waasi wa M23 walipoanza mashambulizi mapya mwezi machi mwaka huu.

 M23 kwa sasa linaudhibiti mji wa Bunagana uliokaribu na taifa la Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.