Pata taarifa kuu
DRC - Rwanda - Usalama

DRC/Rwanda : Yakubaliana kumaliza tofauti zao

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda, zimekubaliana kuanza mchakato wa kumaliza tofauati zao, baada ya mkutano wa marais wa nchi hizo mbili waliokutana jana jijini Luanda nchini Angola.

Marais wa Rwanda Paul Kagame, João Lourenço wa Angola na Félix Tshisekedi wa Kongo wakati wa mkutano wao wa tatu kutafuta suluhu mjini Luanda, Julai 6, 2022, kuhusu mvutano mashariki mwa DRC
Marais wa Rwanda Paul Kagame, João Lourenço wa Angola na Félix Tshisekedi wa Kongo wakati wa mkutano wao wa tatu kutafuta suluhu mjini Luanda, Julai 6, 2022, kuhusu mvutano mashariki mwa DRC AFP - JORGE NSIMBA
Matangazo ya kibiashara

Msuluhishi wa mvutano wa wiki kadhaa kati ya nchi hizo jirani, rais wa Angola Joao Lourenco, ametangaza kuwa pande mbili zimekubaliana kusitisha mvutano kati, bila ya kueleza  kwa undani wa kilichoafikiwa.  

Hata hivyo, Ofisi ya rais Felix Thisekedi, kupitia msemaji wake Erick Nyindu amesema watahakikisha makubaliano yalioafikiwa  yanatekelezwa kwa lengo la kupata amani Mashariki mwa DRC na kwamba kuna matumaini    uhusiano kati ya Rwanda na DRC  utaimarika tena, Nyindu akiongeza kuwa DRC, itahakikisha  wakimbizi hasa wa FDLR na wengine  wanarudi wanarejeshwa Rwanda.

 Aidha, ripoti zinaeleza kuwa mkutano huo ulikuja na mambo sita ambayo nchi hizo zinataka yatekelezwa ikiwemo kurejesha uhusiano wa kidiplomasia lakini pia kuacha kutumia makundi ya waasi ya M 23 na  FDLR kutishia usalama wa nchi hizo mbili.

Kamati ya pamoja kati ya DRC na Rwanda itaundwa kuhakikisha uteketelezwaji wa mambo yaliyokubaliwa na inatarajiwa kukutana jijini Luanda tarehe 12 mwezi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.