Pata taarifa kuu
BURUNDI

UN: Hali ya haki za binadamu bado yatia wasiwasi Burundi

Tume ya uchunguzi, iliyoteuliwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, iliwasilisha ripoti yake ya tano Jumatano, Septemba 15. Tume hiyo ya uchunguzi ilianzishwa mnamo 2016.

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye
Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye AFP Photos/Tchandrou Nitanga
Matangazo ya kibiashara

Jukumu lake hapo awali lilikuwa kuandika visa vya ukiukaji wa haki za binadamu na unyanyasaji uliofanywa nchini Buruni Aprili 2015, wakati wa maandamano ya kwanza dhidi ya kuchaguliwa tena kwa rais wa zamani Pierre Nkurunziza. Tangu wakati huo Évariste Ndayishimiye alichukuwa mikoba yake mnamo Juni 2020.

Kazi ya hivi karibuni ya tume hiyo ya uchunguzi inaonyesha mabadiliko kidogo tangu kuapishwa kwa rais huyo mpya.

Doudou Diène, mwenyekiti wa tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Burundi, alibaini wazi hatua kadhaa kadhaa zilizzopigwa na serikali mpya, kama vile kuachiliwa kwa baadhi ya waandishi wa habari na wanaharakati wa haki za binadamu. Lakini kwake, hii haitoshi: "Tangu kuapishwa kwa rais Ndayishimiye, tume inaona kuwa kunaendelea kuripotiwa visa vya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, ambavyo vingine zinaweza kusababisha uhalifu dhidi ya binadamu, na pia kuzuia kukuwa kwa demokrasia na kuendelea kukataa kwa viongozi wa Burundi kufanya mazungumzo kuhusu maswala ya haki za binadamu. "

Kutowachukulia hatua wale wanaohusika na visa vya unyanyasaji

Sababu nyingine inayotia wasiwasi tume ya uchunguzi ni madai ya kutowaajibisha wale wanaohusika na mateso, mauaji au visa vya watu kutoweka. Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wanahusisha visa hivyo Imbonerakure, kundila vijana wa chama tawala, na idara ya ujasusi.

Ili hali ibadilike nchini Burundi, mabadiliko yanahitajika katika sekta mbalimbali, kulingana na Françoise Hampson, mjumbe wa kamati: "Hatuwezi kusema juu ya dhamana ya haki za binadamu. Inategemea nia ya rais, ikiwa anataka kukuachilia huru, unaachiliwa, lakini hiyo sio sheria kwa nchi yenye haki. Ili kuwa na sheria inayofanya kazi kwa nchi yenye haki na mfumo wa ufadhili wa serikali na mfumo wa kimahakama unaofanya kazi, kunahitajika mabadiliko ya muundo na hadi sasa hatuoni chochote kilichofanywa. Ripoti zetu zinaweza kuwasaidia washirika wa Burundi na jamii ya kimataifa kutambua ni wapi wanaweza kusaidia Burundi kusonga mbele, lakini hiyo inategemea kwanza na nia njema ya serikali, na hadi sasa hatujaona mabadiliko yoyote ya muundo. "

Mageuzi kidogo

Tangu tume ya Umoja wa Mataifa ichunguze hali ya haki za binadamu nchini Burundi, ripoti zake zinaonyesha mabadiliko kidogo. Wanachama wanakumbuka kuwa jukumu lao sio kuchochea mapinduzi, lakini kutaja visa vyote vya ukiukaji kwa historia na haki.

Ripoti hii itawasilishwa kwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa Alhamisi ya wiki ijayo. Ni nchi wanachama ambao ndio wataamua ikiwa muda wa tume ya uchunguzi juu ya Burundi utaongezwa au la kwa mwaka wa sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.