Pata taarifa kuu
UGANDA-USALAMA

Uganda: Mji wa Masaka wakumbwa na visa vingi vya mauaji

Tangu mwezi Julai, angalau watu 28 wameuawa kwa mapanga na wahalifu katika mji wa Masaka na katika wilaya ya Lwengo, ngome kuu ya upinzani katikati mwa Uganda.

Barabara kuu ya jiji la Masaka, Uganda.
Barabara kuu ya jiji la Masaka, Uganda. © CC BY-SA 3.0/Wikimedia Commons/Hectorzalazar
Matangazo ya kibiashara

Wahanga wa mauaji hayo ni wazee, kulingana na polisi, ambayo inasema inawashikilia watuhumiwa 20. Hakuna sababu ya mauajihayo ambayo imetolewa.

Mashambulizi ya mwisho ya aina hii yalitokea miaka mitatu iliyopita, na kufikia sasa, wakazi wa maeneo hayo wapepandwa na hasira kufuatia mauaji hayo yaliyokithiri.

Tangu mwishoni mwa mwezi Agosti, raia wa Uganda wanaandamana kudai haki kwa waathirika wa mfululizo huu mpya wa mauaji chini ya kauli mbiu "wakaazi wa Masaka wana haki ya kuishi".

Ni kwa ujumbe huu ambao mwanasiasa wa upinzani Stella Nyanzi alitaka kuelezea Alhamisi wakati wa maandamano haya. Aliikosoa polisi kwa kutowajibika kwake, kauli  ambayo inaonekana polisi haikufurahia. Aliporudi nyumbani kwake, Nyanzi alikuta maafisa wengi wa polisi wakimsubiri.

"Sielewi kwa nini watu waliojihami kwa bunduki aina ya Kalashnikov, vijiti na mabomu ya machozi wameingia nyumbani kwangu, walikuwa pia mbwa kubwa. Niliwaambia: "Angalia, wakazi wa Masaka wamechoka kuona wauaji hawa wanabebelea mapanga halafu hakuna mnachokifanya. Ikiwa unataka kweli kuonyesha ujasiri wenu, muwadhibiti wauaji wa raia hawa wa Uganda wasio na na hatia, hakuna mtu mnayekuja kukamata nyumbani kwa wazazi wangu ".

Watuhumiwa thelathini walikamatwa, lakini hiyo haikuzuia mauaji. Polisi wanawatuhumu wakaazi wa Masaka kutotoa ushirikiano wao. Mamlaka inaamini kwamba uhalifu huu umepangwa.

Jumanne wiki hii , Rais wa Uganda Yoweri Museveni alibaini kwamba wanaoagiza kutekelezwa kwa mauaji hayo ni waasi wa ADF kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Museveni pia aliomba msaada kutoka mamlaka ya DRC kuwapata viongozi wa kundi hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.