Pata taarifa kuu
Somalia-AMISOM

Majeshi ya Sierra Leone na Djibouti kujiunga na AMISOM nchini Somalia

Mataifa ya Sierra Leone na Djibouti yanatarajiwa, kutuma wanajeshi wa kulinda usalama nchini Somalia katika majuma machache zijazo.

Majeshi ya AMISOM yakipiga doria kwenye bandari ya Mogadiscio.
Majeshi ya AMISOM yakipiga doria kwenye bandari ya Mogadiscio. (Photo : Stéphanie Braquehais/RFI)
Matangazo ya kibiashara

Hii ni baada ya mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Jean Ping kuwasili nchini Somalia, na kushauriana na serikali ya mpito kuhusu mpango wa kuwatuma askari hao nchini humo. Taifa hilo la Somalia, linakumbwa na machafuko ya kikabila yaliosababisha kukosekana kwa serikali inayokubalika na pande zote na yenye nguvu.

Machafuko ya hapa na pale, ndio yaliopelekea Umoja wa Mataifa kuyatuma majeshi yake nchini humo kuisaidia serikali hiyo dhaifu. Burundi na Uganda ndizo nchi ambazo ziliyatuma majeshi yake nchini Somalia kuisaidia nchi hiyo kujikwamua kuondoka katika lindi la machafuko ya wenyewe kwa wenye.

Kundi la Al Shabab linalothibiti eneo kubwa la nchi hiyo, limekuwa likipambana na wanajeshi wa serikali wakisaidiwa na wa Umoja wa Afrika nchini humo AMISOM.

Hali hiyo ngumu ya vita vya hapa na pale imesababisha wananchi kutoroka ma kwao baadhi kukimbilia ugenini huku wengine wakijikuta katika maeneo yenye ukame na hivyo kukabiliwa na janga la njaa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.