Pata taarifa kuu
UHURU WA KUJIELEZA

Tume ya Haki za Kibinadamu ya UN yashtumu ukosefu wa uhuru wa kujieleza Sudan Kusini

Sudan Kusini haiko tayari kwa uchaguzi wa mwaka wa 2024. Hili ni hitimisho la ripoti ya Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu, iliyochapishwa Alhamisi Oktoba 5. Hata hivyo, hili ndilo linalotolewa na makubaliano hayo yaliyohuishwa, ambayo mwaka 2018 yalimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Salva Kiir, ambaye bado yuko madarakani, na Riek Machar, makamu wake wa zamani wa rais.

Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa mnamo Novemba 2022.
Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa mnamo Novemba 2022. © VALENTIN FLAURAUD / AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kikanda, Gaëlle Laleix

Kulingana na ripoti ya Tume ya Haki za binadamu, Sudan Kusini haitoi "mazingira mazuri kwa demokrasia" kwani inapinga mjadala wowote. Ripoti hiyo inaangazia mfumo wa ukandamizaji, hasa wa vyombo vya habari, uliowekwa na serikali ya Sudan Kusini.

Katika mfumo huu, idara ya Usalama ya kitaifa (NSS) inanyooshewa kidole. NSS inarekodi, inasikiliza, inafuata, inatishia na kuwafunga waandishi wa habari. Mnamo mwezi Agosti 2022, mwandishi Diing Magot alikamatwa mchana kweupe baada ya kuwahoji wanafunzi. Akituhumiwa kwa ujasusi, alikaa kizuizini kwa siku nane bila kufunguliwa mashtaka yoyote dhidi yake. Mnamo mwezi Januari 2023, waandishi wa habari 7 kutoka kituo cha SSBC walipelekwa kwenye makao makuu ya NSS. Wengine walizyuiliwa kwenye makao makuu ya NSS hadi mwezi Machi.

Katika vyumba vya habari, afisa aliye na uhusiano na NSS anasoma au kukagua habari kabala ya kuchapishwa au kutangazwa, na anakataa kuchapishw au kutangazwa mada nyeti: upinzani, haki za binadamu, maisha ya kisiasa kwa ujumla. Chini ya masharti haya, vyumba vingi vya habari hujiwekea kikomo kwa kuangazia matukio rasmi pekee, ripoti hiyo inabainisha. Lakini hata katika matukio haya, waandishi wa habari wakati mwingine hujikuta wakitishiwa na Waziri wa Habari. "Kuachana na vitendo hivi vya kiimla itakuwa muhimu kama Wasudan Kusini watatimiza matarajio yao ya uhuru," anahitimisha Barney Afako, mmoja wa makamishna wa Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.