Pata taarifa kuu

Sudan Kusini: Viongozi watakiwa kuheshimu mkataba wa amani

NAIROBI – Balozi maalumu wa umoja wa Mataifa kwa nchi ya Sudan Kusini, Nicholas Haysome, ameliambia baraza la usalama la umoja wa Mataifa kuwa, ni lazima viongozi wa taifa hilo waoneshe uwajibikaji katika kutekeleza mkataba wa amani, vinginevyo kuna hatari ya nchi hiyo kurejea tena katika vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir REUTERS - JOK SOLOMUN
Matangazo ya kibiashara

Licha ya kukosoa kasi ndogo ya utekelezwaji wa mkataba wenyewe, Haysome, alieleza kurudhishwa na juhudi za nchi za ukanda katika kuhakikisha uchaguzi wa mwakani unafanyika kwa wakati.

“Uongozi wa Sudan Kusini kwa sasa unakabilwa na hali ya kuchaguwa njia gani watumie wanaweza kuamua kutumia njia ya ushirikiano na maridhiano katika uharaka wa kutekeleza mkataba wao wa amani au wanaweza kutumia njia fupi inayoweka kando masilahi binafsi au vurugu dhidi ya ujenzi wa taifa.”ameeleza Nicholas Haysome.

Hatua ya rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, kumfuta kazi waziri wa ulinzi na yule wa mambo ya ndani, imeendelea kuibua mjadala kuhusu hatma ya utekelezaji wa mkataba wa amani uliotiwa saini na viongozi wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa mkataba wa amani wa mwaka 2018, ambao haujatejelezwa kikamilifu, nafasi ya Waziri wa Ulinzi inapaswa kutolewa kutoka upanda wa Machar. 

Hata hivyo, Kiir amekiuka mkataba huo na kuamua kuwa Waziri ajaye wa Ulinzi atatoka kwenye chama chake huku ule wa usalama wa ndani atatoka upande wa Machar. 

Msemaji wa Puok Both Baluang, wiki hii ameeleza kuwa mabadiliko hayo yanakwenda kinyume na mkataba wa amani, unaoweza kusababisha changamoto katika serikali ya pamoja kati ya Kiir na Machar katika siku zijazo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.