Pata taarifa kuu

Bwawa la Renaissance: Misri na Ethiopia zinajipa miezi minne kupata makubaliano

Mkutano ambao haujawahi kushuhudiwa ulifanyika kando ya mkutano wa kilele wa Cairo wa nchi jirani za Sudan siku ya Jumatano: mkutno wa Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed. Nchi zao mbili zimekuwa katika mzozo kwa zaidi ya miaka kumi kuhusu suala la bwawa la Grand Ethiopian Renaissance Dam (Gerd) lililojengwa kwenye Mto Blue Nile.

Rais wa Ethiopia Abiy Ahmed akipeana mkono na mwenzake Abdel Fattah al-Sissi Julai 13, 2023 mjini Cairo.
Rais wa Ethiopia Abiy Ahmed akipeana mkono na mwenzake Abdel Fattah al-Sissi Julai 13, 2023 mjini Cairo. © Présidence égyptienne via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Ilichukua mikutano miwili ya ana kwa ana, mmoja Jumatano jioni na mwingine baada ya mkutano wa kilele wa Sudan siku ya Alhamisi. Hatimaye, Abdel Fattah al-Sissi na Abiy Ahmed walitangaza kwamba, kwa kutumia maneno ya taarifa yao ya pamoja kwa vyombo vya habari, "wamepata njia ya kuvunja mvutano uliopo".

Kwa hakika, baada ya miaka mingi ya mvutano na kutoelewana, wawili hao wamekubali, "kuanza mazungumzo ya haraka ili kukamilisha makubaliano kati ya Misri, Ethiopia na Sudan", nchi tatu zinazochangia Mto Blue Nile ambao bwawa hilo linapatikana, inasema taarifa hii kwa vyombo vya habari. Hapo awali, Misri ilibaini kuwa inakabiliwa na "tishio lililopo" na mabadiliko ya mtiririko wa mto unaohusishwa na bwawa.

Majadiliano juu ya awamu ya nne ya ujazo

Kitakachojadiliwa ni awamu ya nne ya ujazo wa bwawa hilo, awamu ya nne iliyotangazwa na Ethiopia mwishoni mwa mwezi Juni, lakini ilisitishwa wiki iliyopita ili kutoa fursa ya mazungumzo. Hatimaye, Misri na Ethiopia zinajitolea kufanya "juhudi zote zinazohitajika kukamilisha makubaliano haya katika muda wa miezi minne", inasema taarifa yao kwa vyombo vya habari.

Tangu mwaka 2020, vita vya maneno viliongezeka hadi suala hilo lilijadiliwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Rais wa Misri alikuwa amewaonya hata wale aliowaita "ndugu zake nchini Ethiopia", akiwaonya kwamba "chaguzi zote" zilikuwa "wazi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.