Pata taarifa kuu
CHINA- AFRIKA- UHUSIANO

Waziri wa mambo ya nje wa China yuko ziarani barani Afrika

Waziri mpya wa Mambo ya nje wa China, Qin Gang amewasili nchini Ethiopia kwa ziara ya wiki nzima katika mataifa matano ya bara la Afrika.

 Qin Gang, waziri wa mambo ya kigeni wa China
Qin Gang, waziri wa mambo ya kigeni wa China © AFP
Matangazo ya kibiashara

Qin, ambaye kabla ya kuteuliwa kwake katika nafasi hiyo, alikuwa Balozi wa China nchini Marekani, anazuru Ethiopia, Gabon, Angola, Benin na Misri, ziara ambayo itatamaliza tarehe 16.

Akiwa jijini Cairo, atakutana na kufanya maazungumzo na Katibu mkuu wa muungano wa nchi za kiarabu.

Kiongozi huo anatarajiwa pia kuzuru mataifa ya Gabon, Angola, Benin na Misiri baada ya kukamilisha kikao cha nchini Ethiopia.

Akiwa nchini humo,waziri  huyo ameratibiwa kufanya kikao na uongozi wa AU.

Ziara hii, ni mwendelezo wa China kuendelea kuyashawishi mataifa ya Afrika, kuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia jambo ambalo limekuwa likiendelea kwa miaka 30 sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.