Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Ethiopia kuzindua awamu ya nne ya kujaza bwawa lake kubwa kwenye Mto Nile

Ethiopia inajiandaa kuzindua awamu ya 4 ya kujaza hifadhi ya bwawa yake kubwa kwenye Mto Blue Nile, naibu waziri wake mkuu ametangaza siku ya Alhamisi, licha ya upinzani wa mara kwa mara kutoka kwa Misri kuwa na wasiwasi juu ya usambazaji wake wa maji chini ya mkondo.

Mwishoni mwa awamu ya tatu ya ujazo, iliyokamilika mwezi Agosti mwaka uliyopita, hifadhi hii ilikuwa na m3 bilioni 22 za maji kati ya bilioni 74 ya uwezo wake kamili.
Mwishoni mwa awamu ya tatu ya ujazo, iliyokamilika mwezi Agosti mwaka uliyopita, hifadhi hii ilikuwa na m3 bilioni 22 za maji kati ya bilioni 74 ya uwezo wake kamili. radioalgerie.dz
Matangazo ya kibiashara

"Awamu ya nne ya ujazo wa Gerd (Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance) unakaribia. Awamu tatu za kwanza za ujazo hazijadhuru nchi zajirani zinazochangia (mto) huo. Ujazo mwingine hautakuwa tofauti," amebaini Demeke Mekonnen wakati akifungua mkutano wa 2 wa Kikanda wa Matumizi Sawa na Yanayofaa ya Mto Nile huko Addis Ababa. "Mkutano huo ambao ulizinduliwa mwaka jana kama "Jukwaa la mazungumzo kati ya wataalamu na wadau", utakuwa mwaka huu na "maafisa wa ngazi juu kutoka wizara mbalimbali".

Mbali na Bw. Demeke, pia Waziri wa Mambo ya Nje, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudan Kusini na Tanzania wanashiriki, nchi zote zinazopakana na Mto White Nile unaoungana na Blue Nile nchini Sudan na kuunda Mto Nile.

Lakini Sudan wala Misri, nchi mbili zinazopatikana chini ya bwawa la Ethiopia kwenye Blue Nile, ahazijawakilishwa. Khartoum na Cairo zimeiomba mara kwa mara Ethiopia kuacha kujaza hifadhi ya Gerd, ikisubiri makubaliano ya pande tatu kuhusu mbinu za uendeshaji wa bwawa hilo, ambalo ni kubwa zaidi barani Afrika.

Wakati Misri, ambayo inategemea Mto Nile kwa karibu 97% ya mahitaji yake ya maji, inaendelea kuomba haki ya kihistoria ya mto huo na kudai kwamba Gerd inaleta tishio "lililopo", msimamo wa Khartoum umebadilika miaka hii iliyopita.

'Kukubaliana kwa pointi zote'

Baada ya miezi kadhaa ya mapambano ya pamoja na Misri mnamo 2022, wakati awamu ya tatu ya kujaza Gerd inakaribia, kiongozi wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, alisema mwezi Januari mwaka huu  "kukubaliana juu ya mambo yote" na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kuhusu Gerd. Lakini Sudan inakumbwa tangu katikati ya mwezi Aprili na mzozo mbaya.

Ipo takriban kilomita thelathini kutoka mpaka wa Sudan, urefu wa kilomita 1.8 na urefu wa mita 145, Gerd hii "inakaribia kukamilika, ikipuuza matamshi ya baadhi ya watendaji wanaotaka kuhodhi matumizi ya mto wa kawaida wa Afrika," Mekonnen aliendelea. "Tuna uhakika kwamba Gerd ina manufaa makubwa kwa nchi za chini ya mto. Hata hivyo mlango wetu unabaki wazi kujibu wasiwasi ambao nchi za pembezoni zinaweza kuwa nao," amebainisha.

Mwishoni mwa awamu ya tatu ya ujazo, iliyokamilika mwezi Agosti mwaka uliyopita, hifadhi hii ilikuwa na m3 bilioni 22 za maji kati ya bilioni 74 ya uwezo wake kamili. Mitambo miwili yenye uwezo wa jumla ya MW 750 tayari inafanya kazi, kati ya 13 iliyopangwa, ambayo hatimaye inatakiwa kuzalisha zaidi ya MW 5,000, ambayo inapaswa kufanya uwezekano wa kuongeza maradufu uzalishaji wa umeme wa sasa wa Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.