Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Ethiopia yajigamba kufikia malengo yake kuhusiana na mradi wa kujaza bwawa lake

Ethiopia imetangaza kuwa imefikia malengo yake ya mwaka wa pili kujaza, bwawa lake kubwa kwa kutumia maji ya Mto Nile, kuendelea na mradi wa kuzalisha umeme, ambao umeendelea kuzua wasiwasi kati yake na nchi za Misri na Sudan.

Ujenzi wa Bwawa hilo, ulioanza mwaka 2011 umekuwa kiini cha mvutano kati ya Ethiopia, Sudan na Misri, huku mataifa hayo mawili yakidai mradi huo utasababisha wanachi wake kushuhudia uhaba wa maji ambayo chanzo chake ni mto Nile.
Ujenzi wa Bwawa hilo, ulioanza mwaka 2011 umekuwa kiini cha mvutano kati ya Ethiopia, Sudan na Misri, huku mataifa hayo mawili yakidai mradi huo utasababisha wanachi wake kushuhudia uhaba wa maji ambayo chanzo chake ni mto Nile. EDUARDO SOTERAS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Maji wa Ethiopia, Seleshi Bekele amethibitisha hatua hiyo na kusema kwa sasa kuna maji ya kutosha kuanza uzalishaji wa umeme.

Hii imekuja baada Ethiopia kuanza harakati za kuanza kujaza bwawa hilo mwaka uliopita, na hatua hii ya pili, imekuja mapema, kinyume na ilivyotarajiwa kuwa ingefanyika kufikia mwisho wa mwezi Agosti.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Waziri huyo wa maji ameeleza kuwa mafanikio hayo yamekuja haraka kufuatia mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha katika eneo hilo.

Ujenzi wa Bwawa hilo, ulioanza mwaka 2011 umekuwa kiini cha mvutano kati ya Ethiopia, Sudan na Misri, huku mataifa hayo mawili yakidai mradi huo utasababisha wanachi wao kushuhudia uhaba wa maji ambayo chanzo chake ni Mto Nile.

Mazungumzo yamekuwa yakiendelea kujaribu kutafuta mwafaka bila mafanikio, huku Ethiopia ikisema inataka mazungumzo hayo kusimamiwa na Umoja wa Afrika na sio Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kama inavyopendekezwa na Sudan pamoja na Misri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.