Pata taarifa kuu
SUDAN

Sudan yataka kukutana na viongozi wa Ethiopia na Misri kutatua mzozo wa Mto Nile

Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok katika mahojiano maalum na Televisheni ya France 24, amesema amewaandikia barua wakuu wa nchi za Ethiopia na Misri, ili kuwa na kikao cha viongozi kutatua mvutano unaoendelea kuhusu bwawa tata la Ethiopia, la kuzalisha umeme linalotumia maji ya Mto Nile.

Ethiopia imeapa kuendelea na mpango wa kujaza bwawa hilo ifikapo katikati ya mwaka huu, hali ambayo inaendelea kuzua wasiwasi kati ya nchi hizo tatu.
Ethiopia imeapa kuendelea na mpango wa kujaza bwawa hilo ifikapo katikati ya mwaka huu, hali ambayo inaendelea kuzua wasiwasi kati ya nchi hizo tatu. © Facebook
Matangazo ya kibiashara

Wito huu wa Hamdok unakuja baada ya mazungumzo kati ya Mawaziri wa mambo ya nje na wale wa maji kukutana wiki iliyopita jijini Kinshasa nchini DRC na kushindwa kufikia mwafaka wowote.

Ethiopia imeapa kuendelea na mpango wa kujaza bwawa hilo ifikapo katikati ya mwaka huu, hali ambayo inaendelea kuzua wasiwasi kati ya nchi hizo tatu.

Ethiopia imjenga Bwa kubwa litakalotegemea mto Nile ili kuzalisha kawi na kuendeleza kilimo lakini Misri inasema bwawa hilo linahatarisha kiwango cha maji kitakachofika Misri na nchi jirani ya Sudan.

Kila nchi inaishtumu nyingine

Ethiopia ilishutumu Misri na Sudan kwa kuzuia mazungumzo juu ya Bwawa la Grand Rianissance la Ethiopia kwenye Mto Nile, ambalo lilimalizika kwa mashtaka ya pande zote na hatua chache kupigwa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia ilisema, katika taarifa kwenye Twitter, kwamba mkutano huo ulishindwa "kwa sababu ya msimamo mkali wa Misri na Sudan katika kufanya mazungumzo na matokeo kuwa chombo cha kudhibitisha sehemu yao ya maji na kuhifadhi sehemu ya Ethiopia'.

"Nchi hizo mbili zimechukua mkakati ambao unatafuta kudhoofisha mchakato unaoongozwa na Umoja wa Afrika," iliongeza taarifa hiyo, na kuongeza kuwa Misri na Sudan zilitaka kuchelewesha na "kuzuwia mchakato" kwa kukataa rasimu ya taarifa hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.