Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-UNSC-AU

Ethiopia yapinga Umoja wa Mataifa kujadili mradi wake wa umeme

Ethiopia imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuheshimu jitihada zinazofanywa na Umoja wa Afrika kutatua mzozo wa kujaza maji kwenye bwawa kubwa la kuzalisha umeme.

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura.
Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura. UN Photo/Loey Felipe
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya nje ya Ethiopia imesema, hatua ya utatuzi wa mzozo huo sio jukumu la Baraza hilo lenye makao yake jijini New York nchini Marekani.

Aidha, Addis Ababa inasema suala hilo sio la Kimataifa na hivyo halipaswi kwenda mbele ya Baraza hilo au muungano wa nchi za kiarabu kulijadili suala hilo.

Naibu Waziri Mkuu Demeke Mekonnen, amesema ni hatari kuondoa mazungumzo hayo kutoka umoja wa Afrika.

Ethiopia imeendelea kuishtumu Sudan na Misri kwa kutafuta wasuluhishi kutoka nje ya Umoja wa Afrika.

Baraza la Usalama la Umoja wa Usalama, linakutana siku ya Alhamisi kujadili mzozo wa matumizi ya maji ya mto Nile, kujaza bwawa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.