Pata taarifa kuu

Burkina Faso: Mamlaka yazuia tani kumi za kuku wasiofaa kuliwa

Nchini Burkina Faso, shirika la kitaifa linalopambana dhidi ya Ulaghai (CNLF) linatangaza kwamba limekamata zaidi ya tani kumi za kuku wasiofaa kuliwa, waliotokea Ulaya na kuingizwa kinyume cha sheria nchini Burkina Faso. "Hii inaleta tatizo la usafi wa afya ya umma," amesema Yves Kafando, mratibu katika CNLF.

Kuku waliohifadhiwa.
Kuku waliohifadhiwa. © Marco Verch Professional Photographer/Flickr
Matangazo ya kibiashara

Huenda janga la kiafya liliepukwa kwa urahisi nchini Burkina Faso. shirika la kitaifa linalopambana dhidi ya Ulaghai (CNLF) linatangaza kwamba usiku wa Aprili 8 hadi 9, 2023, ilikamata magari kumi na matatu yaliyokuwa yamebeba zaidi ya tani kumi za kuku wasiofaa kuliwa, sawa na faranga za CFA milioni 100. Bidhaa kutoka Ulaya na ambazo ziliingizwa kinyume cha sheria katika ardhi ya Burkina Faso.

"Unaweza kupata magonjwa kufuatia matumizi ya aina hii ya bidhaa"

Kulingana na Yves Kafando, mratibu wa kitaifa wa CNLF, kuku hawa walikusudiwa kuuzwa kwa wakazi. Lakini matumizi yao yanaweza kuwa hatari sana kwa afya. "Hali za usafiri hazijazingatiwa, amesema akihojiwa na Clémentine Pawlotsky. Ni bidhaa ambazo zili ambazo ziliwekwa kwenye friji na zilipaswa ziagizwe chini ya hali ya joto fulani, ambazo kwa bahati mbaya zimefungwa kwenye magari ambayo hayafai kwa aina hii ya usafiri. Na tulipata kifurushi ambacho kilikuwa kimechanika. Tulikuta baadhi ya kuku wameanza kuyeyuka kwa hivyo kulikuwa na maji yanayotoka. Baadhi ya bidhaa hazikua katika mazingira mazuri”.

Anaongeza: “Lazima isemwe kwamba hii inaleta tatizo la usafi wa afya ya umma. Hii haiwezi kubaki hivyo bila kusababisha madhara kwa afya ya binadamu. Kwa muda mrefu, mtu anaweza kupata magonjwa ambayo yanaweza kuwa mfululizo kwa matumizi ya aina hii ya bidhaa. Lakini hatua yetu ya leo inalenga kulinda raia, kulinda wanunuzi. Na kwa kweli tuna kazi ngumu ya kuweza kusambaratisha mitandao mbalimbali inayoendelea. "

Yves Kafando pia anabainisha kuwa madereva saba walikamatwa. Wengine sita wako mafichoni na hawakuweza kutambuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.