Pata taarifa kuu
MGOMO-AFYA

Wahudumu wa afya wa kijeshi watumwa katika hospitali za Afrika Kusini zilizo katika mgoma

Wahudumu wa afya wa kijeshi wametumwa katika hospitali kadhaa za umma nchini Afrika Kusini ili kupunguza madhara ya mgomo ambao serikali inasema umesababisha vifo vya watu kadhaa, jeshi limebaini siku ya Jumatatu.

Wagonjwa wakiwa kwenye foleni katika Hospitali ya Tintswalo katika Mkoa wa Mpumalanga, kaskazini mashariki mwa Afrika Kusini, Agosti 2007.
Wagonjwa wakiwa kwenye foleni katika Hospitali ya Tintswalo katika Mkoa wa Mpumalanga, kaskazini mashariki mwa Afrika Kusini, Agosti 2007. AFP / Isaac Mangena
Matangazo ya kibiashara

"Tumepokea ombi kutoka kwa Waziri wa Afya kusaidia katika mgomo unaoendelea na kuhakikisha kuwa huduma zinafanya kazi bila usumbufu wowote," msemaji Phillip Makopo ameliambia shirika la habari la AFP.

"Wataalamu wa afya wa kijeshi walitumwa katika hospitali mbalimbali Jumatano" ya wiki iliyopita na "watabakia pale hadi itakapohitajika," amesema.

Waziri wa Afya wa Afrika Kusini Joe Phaahla amesema takriban wagonjwa wanne wamefariki na kwamba vifo vyao "vinaweza kuhusishwa moja kwa moja na mgomo huo". Wiki iliyopita, wagomaji walizuia watu kufika katika hospitali mbalimbali.

Siku ya Jumatatu asubuhi, waandishi wa habari wa AFP waliona askari wanne wakiwa wamekaa karibu na Hospitali ya Thelle Mogoerane kusini mashariki mwa Johannesburg, huku polisi wakishika doria kwenye lango la kuingilia.

Mgomo huo unaoathiri hospitali kadhaa za umma ulianza wiki moja iliyopita kwa kusimamishwa kazi kwa wafanyakazi wa wauguzi na wafanyikazi wa matengenezo wakidai nyongeza ya 10% ya mishahara yao, huku serikali ikikubali tu 4.7% ya nyongeza.

Siku ya Jumatatu, mahakama iliamuru kusitishwa kwa momo huo lakini wagomaji wanaendelea kupuuzia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.