Pata taarifa kuu
ULINZI-DIPLOMASIA

Afrika Kusini: Mazoezi ya kijeshi na China na Urusi yazua sintofahamu

Zoezi la Mosi 2 litazinduliwa Ijumaa hii, Februari 17 nchini Afrika Kusini. Chini ya jina hili la msimbo, ambalo linamaanisha "moshi" katika lugha ya Kisotho, huficha mazoezi ya kijeshi yatakayofanywa Durban, Mashariki, kwa pamoja na China na Urusi. 

Wanajeshi wa jeshi la Afrika Kusini wakitazama umati wa watu huko Vosloorus, mashariki mwa Johannesburg, Julai 14, 2021.
Wanajeshi wa jeshi la Afrika Kusini wakitazama umati wa watu huko Vosloorus, mashariki mwa Johannesburg, Julai 14, 2021. AP - Themba Hadebe
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa serikali ya Pretoria, hili si lolote zaidi ya zoezi la kawaida na washirika wake wa BRICS (Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini), kwani nchi hiyo inatetea msimamo wa kutofungamana na upande wowote kuhusu vita vya Ukraine. Lakini kwa washirika wake wa Magharibi, mazoezi haya yanakuja wakati mbaya.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Naledi Pandor, hili ni zoezi jingine linalofanywa na vikosi vya washirika, kama vile nchi hiyo tayari imefanya hivi karibuni na Marekani na Ufaransa: "Nchi zote hufanya mazoezi ya kijeshi na marafiki zao. Hivyo kusiwe na shinikizo kwa taifa lolote kuwalazimisha kufanya hivyo na baadhi ya washirika pekee. Hii ni sehemu ya kawaida ya uhusiano kati ya nchi. "

Mazoezi haya ya pamoja ya kijeshi kati ya Afrika Kusini, China na Urusi yamepangwa kwa muda mrefu, lakini yanakuja wakati mbaya, wakati tarehe ambayo ni ishara ya kuanza kwa vita huko Ukraine. Kwa upande wa chama kikuu cha upinzani, Democratic Alliance, na mmoja wa wawakilishi wake, Kobus Marais, kinasema serikali ilipaswa kufuta mazoezi haya: "Ni upumbavu na kutowajibika. Afrika Kusini inacheza nafasi ya mjinga muhimu katika zoezi hili la wazi la propaganda za Urusi dhidi ya vikosi vya Magharibi. "

Kwa hivyo Pretoria inasalia katika usawa wake, kulingana na Jo-Ansie van Wyk, profesa wa siasa za kimataifa katika Chuo Kikuu cha Afrika Kusini: "Nchi inataka kudumisha uhusiano wake wa kiuchumi na Kaskazini, lakini pia inapenda kuanzisha utaratibu mpya wa kimataifa. Na Urusi na China ni washirika wazuri kwa Afrika Kusni, wakishiriki itikadi hii. »

Meli kubwa ya kijeshi ya Urusi , Admiral Gorshkov, itashiriki katika mazoezi haya, bila kuwa na uhakika kwa sasa kwamba makombora yake ya Zircon hypersonic yatapigwa kwa ajili ya majaribio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.