Pata taarifa kuu
DIPLOMASIA-ULINZI

Afrika Kusini kupokea Urusi na China kwa mazoezi ya kijeshi ya majini

Afrika Kusini, ambayo mara zote imekataa kulaani Urusi kwa uvamizi wake nchini Ukraine, imetangaza leo Alhamisi kufanyika kwa mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya majini mnamo mwezi Februari na jeshi la wanamaji la Urusi na China kwenye pwani yake.

Kufuatia mwaliko wa Pretoria, jeshi la wanamaji la Urusi litashiriki mazoerzi ya kijeshi ya pamoja katika pwani ya Afrika Kusini mwezi Februari.
Kufuatia mwaliko wa Pretoria, jeshi la wanamaji la Urusi litashiriki mazoerzi ya kijeshi ya pamoja katika pwani ya Afrika Kusini mwezi Februari. AFP PHOTO / MAX VETROV
Matangazo ya kibiashara

"Afrika Kusini itakuwa itapokea jeshi la wanamaji la China na lile la Shirikisho la Urusi wakati wa mazoezi ya baharini kati ya Februari 17 na 27," jeshi la Afrika Kusini limethibitisha katika taarifa.

"Ili kuimarisha uhusiano ambao tayari umeshamiri kati ya Afrika Kusini, Urusi na China", luteka hii ya kijeshi ya pamoja itafanyika kwenye pwani ya Durban, bandari kubwa zaidi kusini mwa Afrika, na kwenye pwani ya Richards Bay kilomita 180 kaskazini, imesema taarifa hii kwa vyombo vya habari.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa zoezi la aina hiyo kufanyika ambalo litashirikisha vikosi hivyo vitatu vya wanamaji, ambapo la kwanza lilifanyika Novemba 2019 huko Cape Town, Afrika Kusini.

Mazoezi haya ya kijeshii yatawaleta pamoja zaidi ya wanajeshi 350 wa Afrika Kusini "kutoka huduma na vitengo kadhaa" pamoja na 'wenzao wa Urusi na China ili kubadilishana ujuzi', taarifa kwa vyombo vya habari imebainisha.

Afrika Kusini, moja ya mataifa yenye nguvu katika bara la Afrika, imechukua msimamo wa kutoegemea upande wowote tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari 24, ikikataa kujiunga na wito wa nchi za Magharibi kulaani Moscow.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.