Pata taarifa kuu
ETHIOPIA- USALAMA- UCHUKUZI

Abiria washindwa kusafari katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia

Nchini Ethiopia, baada ya kurejelewa kwa safari za ndege kutoka jiji kuu Addis Ababa hadi mji wa jimbo la Tigray, Mekelle, abiria wengi wameshindwa kusafiri kwa kushindwa kutimiza masharti yaliyotangazwa na Shirika la ndege la nchi hiyo.

Ndege ya shirika la ndege la Ethiopia
Ndege ya shirika la ndege la Ethiopia AP - Elias Asmare
Matangazo ya kibiashara

Kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita, baadhi ya abiria waliofika katika uwanja wa ndege wa Mekelle kwenda Addis Ababa, walizuiwa kusafiri, hasa wakiwa na umri kati ya miaka 16 hadi 65.

Shirika la ndege la Ethiipia, halijaeleza ni kwanini sharti hilo limewekwa na ni nani alitoa maagizo hayo, hatua ambayo imewafanya wengi kushindwa kusafiri.

Kutoka Mekelle ni watoto tu na watu wenye umri zaidi ya miaka 65, ndio wanaoruhusiwa kuondoka au mtu mwenye cheti cha daktari kuonesha kuwa, wanahitajika kupokea matibabu jijini Addis Ababa.

Uongozi wa Tigray umesema haujaweka masharti hayo, wakati huu maeneo mengi ya jimbo hilo na mji wa Mekelle ukiwa chini ya usalama wa maafisa wa serikali kuu.

Utulivu kwa sasa unashuhudiwa jimboni Tigray, baada ya pande zilizokuwa zinazozana waasi wa jimbo hilo na serikali ya Addis Ababa kutia saini mkataba wa amani mwezi Novemba mwaka ulipita, jijini Pretoria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.