Pata taarifa kuu

Afrika Kusini yaomboleza kifo cha Spika wa Bunge la kwanza lililochaguliwa kidemokrasia

Mwanaharakati aliyepambana dhidi ya ubaguzi wa rangi Frene Ginwala, ambaye alikuwa spika wa Bunge la kwanza la Afrika Kusini lililochaguliwa kidemokrasia na mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90, ofisi ya rais wa Afrika Kusini imetangaza siku ya Ijumaa.

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa. AFP
Matangazo ya kibiashara

Alifariki akiwa nyumbani kwake Alhamisi jioni baada ya kuugua kiharusi wiki mbili zilizopita. "Leo tunaomboleza kifo cha mzalendo wa kutisha," Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema katika taarifa yake.

"Tumepoteza mtu mwingine mkubwa na muhimi kati ya kizazi cha kipekee cha viongozi ambao walitetea uhuru wetu na ambao tunawajibika kwao kuendelea kujenga Afrika Kusini baada ya kujitolea kwa kila kitu," ameongeza.

Frene Ginwala aliteuliwa kuwa Spika wa Bunge mwaka 1994, huku Nelson Mandela akichaguliwa kuwa rais, na hivyo kuashiria mwisho wa utawala wa kibaguzi. Alishikilia nafasi hii hadi mwaka 2014.

"Haki nyingi na faida walizo nazo Waafrika Kusini leo yana chimbuko lao katika mpango wa kutunga sheria wa bunge la kwanza la kidemokrasia chini ya uongozi wa Dk Ginwala," Rais Ramaphosa amebainisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.