Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Wajumbe wa chama cha ANC kumchagua kiongozi mpya

Wajumbe wa chama tawala  cha ANC nchini Afrika Kusini, wanapiga  kura kumchagua rais mpya wa chama hicho, wakati huu rais Cyril Ramaphosa ambaye amekumbwa na madai ya ufisadi akitarajiwa kuchaguliwa. 

Mjumbe wa ANC akiwa katika mkutano mkuu wa chama, Desemba 16 2022
Mjumbe wa ANC akiwa katika mkutano mkuu wa chama, Desemba 16 2022 AFP - GUILLEM SARTORIO
Matangazo ya kibiashara

Walianza mkutano mkuu siku ya Ijumaa, huku Ramaphosa akieleza kuwa ana imani ya kuchaguliwa tena, baada ya wabunge wiki hii kutupilia mbali, ripoti iliyokuwa inamtuhumu kwa  madai ya wizi wa fedha za umma.

Wakati wa hotuba yake ya ufunguzi, Ramaphosa alizomewa na wafuasi wa rais wa zamani, Jacob Zuma, aliyeondolewa madarakani kwa madai ya ufisadi.

Mpinzani wa Ramaphosa kwenye uchaguzi huu ni Zweli Mkhize, aliyekuwa Waziri wa afya, ambaye pia anatuhumiwa, kuhusika na wizi wa fedha za kupambana na janga la Covid 19.

Kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2024, chama cha ANC ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka 1994 baada ya kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi, katika miaka ya hivi karibuni, imekubwa na visa vya ufisadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.