Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Rais Ramaphosa ateuliwa tena kukiongoza chama cha ANC

Chama tawala nchini Afrika Kusini kimemchagua tena Cyril Ramaphosa kama kiongozi wake siku ya Jumatatu, na hivyo kumweka katika nafasi nzuri ya kugombea muhula wa pili wa uongozi ikiwa chama hicho cha kihistoria kitashinda uchaguzi mkuu mwaka 2024.

Cyril Ramaphosa baada ya kuchaguliwa tena kama rais wa chama tawala, Desemba 19, 2022.
Cyril Ramaphosa baada ya kuchaguliwa tena kama rais wa chama tawala, Desemba 19, 2022. REUTERS - SIPHIWE SIBEKO
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mazungumzo na miungano ya dakika za mwisho wikendi iliyopita, Rais Ramaphosa amechaguliwa tena Jumatatu kama mkuu wa chama chake kwa kura 2,476 dhidi ya 1,897 za mpinzani wake, Waziri wake wa zamani wa Afya Zweli Mkhize.

Licha yakuwa juu mwishoni mwa juma hili, wapinzani wa Cyril Ramaphosa, waliounga mkono kugombea kwa Zweli Mkhize, wameonekana wameshindwa. Akiwa na umri wa miaka 70, alishinda kinyang'anyiro hicho kwa zaidi ya kura 500. Ushindi uliosherehekewa na wafuasi wake kwa nyimbo na densi katika kituo cha mikutano cha Johannesburg, vidole viwili vilivyoinuliwa juu kuashiria kuwa muhula wa pili sasa unapatikana.

Matokeo haya ni uthibitisho zaidi kwamba, licha ya suala la "Phala-Phala" na maswali yanayohusu wizi wa fedha zilizofichwa shambani mwake, Cyril Ramaphosa ameweza kudumisha imani ya wenzake, "wenzake" wa chama cha ANC.

Msimamo ulioimarishwa

Na pia atakuwa na uwezo wa kulazimisha timu yake kuwa mkuu wa chama, jambo muhimu kwani wakati wa muhula wake wa kwanza, alilazimika kushirikiana na viongozi wa kambi pinzani. Kati ya nyadhifa saba muhimu zaidi, zilizopewa jina la utani la "7 bora", ni nafasi mbili tu ambazo washirika wake wamekosa, ikiwa ni pamoja na ile ya makamu wa rais.

Muhula huu wa pili wa kiongozi wa ANC kwa hivyo unapaswa kumpa mwanaharakati huyo wa zamani wa vyama vya wafanyakazi na mfanyabiashara fursa zaidi ya kuweka maono yake kwa nchi na kujaribu kuhifadhi wingi kamili wa wabunge wakati wa uchaguzi mkuu wa 2024.

Na chaguo la Cyril Ramaphosa pia linavutia soko, kwani rand imeimarika kwa zaidi ya 2% dhidi ya dola, kufuatia tangazo la kuchaguliwa kwake tena.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.