Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI- SIASA

Ramaphosa kifua mbele kushinda kinyang'anyiro cha kumtafuta rais wa ANC

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, anatazamiwa kushinda katika kinyang'anyiro cha kumtafuta kiongozi mpya wa chama tawala cha ANC.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa AP - Themba Hadebe
Matangazo ya kibiashara

Chama cha ANC hivi leo kimeanza mkutano wa wake wa kitaifa kuchagua uongozi mpya, rais Cyril Ramaphosa akitazamia kuchaguliwa tena kama kiongozi wa chama hicho baada yake kuepuka kura ya kutokuwa na imani naye bungeni.

Mapema wiki hii, wabunge wa ANC walipiga kura kupinga ripoti iliyoonyesha kuwa huenda rais Ramaphosa alikiuka sheria ya kupamabana na ufisada kufuatia wizi wa fedha za kigeni katika shamba lake.

Ramaphosa anatarajiwa kupambanana waziri wa zamani wa afya Zweli Mkhize katika kinyanganyiro hicho cha kumpata kiongozi wa chama cha ANC.

Inatarajiwa kuwa kamati ya nidhamu ya chama hicho itawasilisha ripoti kusuhu sakata la Farmgate linalomhusisha rais ramaphosa lakini pia sakata la ufisadi linalomkabili mpinzani Wake Dkt Mkhize ambaye anadaiwa kufaidika na kandarasi ya serikali ya Uviko 19.

Hata hivyo, Ramaphosa anatarajiwa kuchaguliwa tena licha ya sakata ambazo zimekuwa zikimuandama hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.