Pata taarifa kuu

Meli kubwa ya kijeshi ya Urusi yaegesha nchini Afrika Kusini kwa mafunzo

Meli kubwa ya kijeshi ya Urusi "Admiral Gorshkov" imetia nanga mjini Cape Town siku ya Jumatatu kwa mazoezi ya pamoja ya wanamaji katika pwani ya Afrika Kusini, Balozi mdogo wa Urusi nchini Afrika Kusini ametangaza, huku mafunzo hayo yakikabiliwa na ukosoaji mkubwa.

Meli kubwa ya kijeshi ya Urusi "Admiral Gorshkov" imetia nanga mjini Cape Town siku ya Jumatatu kwa mazoezi ya pamoja ya wanamaji katika pwani ya Afrika Kusini.
Meli kubwa ya kijeshi ya Urusi "Admiral Gorshkov" imetia nanga mjini Cape Town siku ya Jumatatu kwa mazoezi ya pamoja ya wanamaji katika pwani ya Afrika Kusini. © Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ilitangaza mwezi Januari kupokea kuanzia Ijumaa na kwa siku kumi Wanamaji wa China na Urusi kwa "mazoezi ya pande tatu" na "kuimarisha uhusiano" kati ya nchi hizo tatu. Pretoria imechukua msimamo wa kutoegemea upande wowote tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari 24, na kukataa kujiunga na wito wa nchi za Magharibi wa kulaani Moscow kwa uvamizi wake dhidi ya Ukraine.

Ubalozi mdogo wa Urusi mjini Cape Town ulichapisha kwenye akaunti yake ya Twitter siku ya Jumatatu picha ya meli hiyo katika bandari ya mji wa pwani, ikisema kuwa iko njiani kuelekea Durban (kusini mashariki). Zaidi ya wanajeshi 350 wa Afrika Kusini watashiriki katika mafunzo yaliyopangwa, hasa katika pwani ya bandari kubwa zaidi katika eneo hilo.

Mazoezi haya ya kijeshi yalishutumiwa vikali na upinzani. "Meli hii itasafiri hadi Bahari Nyeusi na kushiriki katika uvamizi wa Ukraine," Kobus Marais, mwanachama wa chama cha kwanza cha upinzani (DA, Democratic Alliance) ambaye ni mbunge, ameliambia shirika la habari la AFP.

"Afrika Kusini inaweza kuonekana kwa urahisi kama mshiriki katika uhalifu huu wa kivita," alionya, akishutumu serikali ya Afrika Kusini kwa kujiruhusu "kuingizwa kwenye propaganda za Urusi."

Ukihojiwa na shirika la habari la AFP, ubalozi mdogo wa Urusi na ubalozi wa Afrika Kusini haukutoa maoni yoyote. Mkuu wa diplomasia ya Ulaya Josep Borrell akiwa ziarani Pretoria mwezi uliopita alizungumzia "mambo ya kuudhi" kuhusu uhusiano wa karibu kati ya Afrika Kusini na Urusi katikati ya vita nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.