Pata taarifa kuu
DRC-AFYA-WAFUNGWA

Mlipuko wa kipindupindu waripotiwa katika Gereza la Goma

Mashirika ya kiraia pamoja na Madaktari wasio na mipaka MSF mkoani Kivu Kaskazini, wameripoti kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu katika Gereza kuu la Goma.

Hali ya mazingira katika Gereza la Goma, Mashariki mwa DRC
Hali ya mazingira katika Gereza la Goma, Mashariki mwa DRC AFP PHOTO/Tony KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Watu wawili wamefariki na wengine zaidi ya 140 wameabukizwa na sasa mashirika ya kiraia mjini Goma, yanaitaka serikali ya Kinshasa kuwahudumia wafungwa hao kama inavyotakiwa.

“Haiwezekani, wafungwa zaidi ya 3,000 kurundikana katika Gereza moja bila ya maji,” amehoji kiongozi wa kiraia John Banyene kiongozi wa kiraia katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Madaktari wasio na mipaka wa MSF, wamethibitisha ugonjwa huo wa kipindupindu kutokea kwenye gerezani hilo na wanaahidi kutoa msaada wa afya.

“Kuna mamabukizi na tumeanza kutoa chanjo na huduma nyingine, “ amesema Jean Paul Kikwayabo kutoka Shirika la MSF.

Nalo shirika lanalojihusisha na maji mjini Goma Regideso, lakini viongozo wa serikali ya Kivu Kaskazini, wakitaka suluhu ya haraka.

 “Tunaomba Serikali,kiongozi wa Regideso hapa Kivu kaskazini na Kinshasa wafanye haraka iwazekanavyo kuleta chakula na madawa gerezani humo na wana nchi wapate Haki Zao ,” amesema Jean Baptiste Kasekwa/

Gereza kuu jijini Goma kwa sasa lina zaidi wafungwa 3,000 huku likiwa na uwezo wa kuchukua watu 150 pekee.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.