Pata taarifa kuu
DRC

Serikali ya Lukonde yatimiza siku 100, mafanikio na changamoto

Serikali ya Waziri Mkuu Sama Lukonde, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inatimiza siku 100 leo Jumatano tangu kuundwa kwake baada ya mvutano mkali kati ya pande mbili, FCC na CASH.

Wanamgambo wakikusanyika huko Ituri, kaskazini mashariki mwa DRC, Septemba 19, 2020.
Wanamgambo wakikusanyika huko Ituri, kaskazini mashariki mwa DRC, Septemba 19, 2020. AFP
Matangazo ya kibiashara

Serikali hiii Iliundwa baada ya kuvunjika kwa muungano ambao Felix Tshisekedi alikuwa ameunda na mtangulizi wake Joseph Kabila. Hatua gani imepigwa kufikia sasa?

Hii ni serikali ya kwanza ya Muungano Mtakatifu, iliyotakiwa na  rais Felix Tshisekedi. Rais wa DRC alijilamu juu ya makubaliano yaliyotiwa saini kati yake na mtangulizi wake. Alimlaumu Joseph Kabila na muungano wake, FCC, kwa kuzuia mageuzi yake, hasa katika nyanja ya haki za binadamu.

Serikali ya Sama Lukonde imepewa jina la "serikali ya pambanaji a mashujaa". Ndani ya siku chache tangu kuuundwa kwake, sheria ya kijeshi ilitangazwa katika mikoa miwili ya nchi hiyo. Chini ya mwezi mmoja baada ya kuapishwa, kulitokea mlipuko wa volcano katika mlima Nyiragong, hali ambayo ilitatiza mpango wa serikali.

Moja ya mafanikio ni kusainiwa kwa makubaliano na Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, ambalo linatarajia kufungua njia ya mageuzi na ulipaji wa dola bilioni moja na nusu kwa zaidi ya miaka mitatu. Rais Tshisekedi alikuwa anataka jambo hilo lifikwe tangu aingie madarakani. Akiba ya fedha za kigeni na ukusanyaji wa mapato vimeboreshwa, lakini kuhusu mabadiliko ya matumizi, hakuna mabadiliko yoyote ya bajeti ambayo yamepitishwa, hali ambayo inasababisha hatua ya serikali hii mpya isiwe wazi. Hii inaweza kushughulikiwa kufikia mwezi Septemba.

Mdororo wa Usalama katika mikoa ya Kaskazini

Kwa vyovyote vile, matarajio ya timu hii bado ni makubwa, hasa katika sekta ya kijamii, kama inavyothibitishwa na mgomo wa kwanza unaoikabili nchi hiyo. Hata hivyo, kutokana na mchakato wa kuteua maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi, CENI, muungano Takatifu unakabiliwa na mafarakano yake ya kwanza.

Waziri Mkuu alikuwa aliahidi kutokomeza makundi ya waasi yanayohatarisha usalama katika mikoa ya Kaskazini, ikiwa ni pamoja na Kivu Kaskazini na Ituri, lakini visa vya utekaji nyara na mauaji bado vinaendelea kuripotiwa, hasa katika mkoa wa Ituri na eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.