Pata taarifa kuu
DRC-WAASI-MAUAJI

Watu 16 wauawa Mashariki mwa DRC, mashirika ya kiraia yalaumu jeshi

Watu 16 wameuawa kwa kuchomwa visu na waasi wanaoaminiwa kuwa wa ADF katika barabara ya Idohu katika mkoa wa Ituri, Mashariki mwa Jamhiuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kutekwa.

Wanajeshi wa kulinda amani wanaopambana na waasi wa ADF Mashariki mwa DRC
Wanajeshi wa kulinda amani wanaopambana na waasi wa ADF Mashariki mwa DRC Photo MONUSCO/Force
Matangazo ya kibiashara

Jeshi na maafisa wa serikali wanasema mauaji hayo yalitokea siku ya Jumatatu na miongoni mwa waliouwa ni wanawake wawili waliokuwa wametekwa wiki kadhaa zilizopita na waasi hao.

Wakati hayo yakijiri, mashirika ya kiraia, yanalalamikia ongezeko la mauaji ya raia katika mkoa huo wa Ituri. Shirika la CEPADHO linasema kwa kipindi cha siku 10 zilizopita, watu 42 wameuawa sawa na wengine 332 wilayani Irumu na wengine 165 huko Beni.

Shirika la LUCHA sasa linataka kuondolewa kwa Gavana wa kijeshi katika jimbo la Kivu Kaskazini linaloongozwa na Constant Ndima kwa mujibu wa kiongozi wa kundi hilo Esai Liko.

Rais anapaswa kumfuta kazi Gavana Ndima kwa sababu ameshindwa kuzuia mateso ya raia. Kila wakati maadui wanaendelea kuwatesa raia na kwenda kinyume cha haki za binadamu.

Upande wa Jeshi, unataka wanaharakati hao kuacha kulalamika na badala yake kusaidia katika mapambano dhidi yta waasi kwa mujibu wa msemaji wa Gavana huyo wa kijeshi, Jenerali Silvain Ekenge.

Kila mmoja analikosoa jeshi, hao vijana wa Lucha wanastahili kujiunga nasi ili kupambana na makundi yanayoendeleza mauaji ya raia.
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.