Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Nigeria: Maswali yaibuka juu ya hatima ya kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau

Kiongozi huyo wa kijihadi anaaminika alijeruhiwa vibaya au labda alifarii unia baada ya kujaribu kujiua ili kutoroka wapiganaji wa Iswap, tawi la Boko Haram linalofungamana na kundi laIslamic State.

Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau azungumza mbele ya walinzi katika eneo lisilojulikana nchini Nigeria katika picha hii iliyopigwa kwa tarehe isiyojulikana na kutolewa Januari 15, 2018.
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau azungumza mbele ya walinzi katika eneo lisilojulikana nchini Nigeria katika picha hii iliyopigwa kwa tarehe isiyojulikana na kutolewa Januari 15, 2018. REUTERS - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Kufikia mwaka 2016, Boko Haram ilikuwa imegawanyika katika makundi mawili: Iswap kwa upande mmoja na kundi la kihistoria ambalo bado linaloongozwa na Abubakar Shekau kwa upande mwingine. Ngome yake ya Sambisa ilishambuliwa Jumatano, Mei 20, na wapiganaji wa kundi la Iswap.

Ripoti za Kiinteljesia zinasema kuwa, kundi la Boko Haram chini ya Shekau limekuwa katika makabiliano na kundi la Islamic State, ISWAP, linaloendeleza harakati zake Afrika Magharibi, katika jimbo la Borno.

Inaelezwa kuwa mapigano hayo yalitokea katika msitu wa Sambisa, kwenye ngome kuu ya Boko Haram, huku wapiganaji wake wakikimbilia kusikojulikana.

Aidha, ripoti nyingine ya kiiteljensia inaeleza kuwa Shekau alijeruhiwa baada ya kushambuliana na wapiganaji wake katika nyumba aliyokuwa amejificha na wapiganaji wake.

Shekau ambaye aligongwa vichwa vya Habari mwaka 2014 baada ya kuwateka wasichana karibu 300 wa shule ya wasichana ya Chibok, na amekuwa akiripotiwa mara kadhaa kuwa aliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.