Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Mahamadou Issoufou: Tunahitaji vikosi zaidi kupambana dhidi ya ugaidi

Rais wa Niger Mahamadou Issoufou amesema kuna umuhimu wa uwepo wa vikosi vya Ufaransa katika vita dhidi ya ugaidi. Kauli hiyo inakuja siku chache baada ya shambulio lililoghaimu maisha ya askari wengi wa Niger.

Mahamadou Issoufou, Rais wa Niger, wakati wa mahojiano na RFI na Ufaransa 24.
Mahamadou Issoufou, Rais wa Niger, wakati wa mahojiano na RFI na Ufaransa 24. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Rais huyo ameyasema hayo Siku nane baada ya kutokea kwa shambulio la kigaidi katika mji wa Inates lililogharimu maisha ya wanajeshi 71.

Katika mahojiano maalum na Gaelle Lailex wa idhaa ya RFI Kifaransa na Cyril Payen wa France 24, rais huyo amesema wanaokosoa uwepo wa vikosi vya Ufaransa katika operesheni dhidi ya Ugaidi wanasahau kwamba bila uwepo wa vikosi hivyo katika operesheni Servalm Mali ingekuwa mikononi mwa magaidi.

Ufaransa imeendelea kukosolewa kutokana na kuendelea kushuhudiwa kwa mashambulizi ya kigaidi ambayo yamegharimu maisha ya wanajeshi wa nchi za ukanda wa Sahel ambapo maandamano dhidi ya wanajeshi wa Ufaransa yameshuhudiwa katika maeneo kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.