Pata taarifa kuu
UFARANSA-SAHEL-USALAMA-USHIRIKIANO

Barkhane: Emmanuel Macron aeleza kinagaubaga kwa marais wa Sahel

Emmanuel Macron ametangaza kwamba atawaalika marais wa nchi tano za Ukanda wa Sahel Desemba 16 kuja katika mji wa Pau Kusini mwa Ufaransa.

Emmanuel Macron kwenye mkutano wa kilele wa NATO, Desemba 4, 2019.
Emmanuel Macron kwenye mkutano wa kilele wa NATO, Desemba 4, 2019. © REUTERS/Christian Hartmann/Pool
Matangazo ya kibiashara

Lengo la mwaliko huo ni kuelezea msimamo wao kuhusu uwepo wa Ufaransa katika ukanda huo, na hiyo inakuja wakati ambapo chuki dhidi ya Ufaransa inaendelea kusambaa katika nchi kadhaa za Ukanda wa Sahel.

Taarifa hii ya rais wa Ufaransa kuhusu uwepo wa Ufaransa katika Ukanda wa Sahel imepokelewa shingo upande wakati wa hitimisho la mkutano wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) Jumatano alasiri wiki hii mjini London, nchini Uingereza.

"Nasubiri wawili wafafanue na kurasimisha ombi lao kwa Ufaransa na jamii ya kimataifa. Mnataka vikosi vya Ufaransa viendelee kuwepo katika Ukanda wa Sahel? Je! Wanatuhitaji? Ninataka majibu ya wazi kwa maswali haya. "

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa ujumbe huu kwa wenzake wa nchi za Ukanda wa Sahel siku tisa baada ya askari 13 wa Ufaransa kufariki dunia katika ajali ya helikopta mbili nchini Mali. Akiwa jijini London, rais wa Ufaransa ametoa wito kwa kila mmoja wa marais hao kuweka wazi msimamo wake kuhusu uwepo wa Ufaransa katika ukanda huo. Kwa wakati huu ambapo chuki dhidi ya Ufaransa inaendelea kukua, chuki ambayo wakati mwingine inachochewa na viongozi wa kisiasa, amesema Emmanuel Macron.

"Tunahitaji waweze kutoa ufafanuzi zaidi na ukweli kuhusu uwepo wetu katika ukanda huo. Kwa sababu Ufaransa haina malengo ya ukoloni mamboleo au malengo ya kiuchumi. Tuko hapo kwa usalama wa pamoja wa ukanda huo na ukanda wetu. Mfumo huu lazima uwe wazi na kuwekwa wazi na kila mtu. Kwa sasa, hiyo haitoshi, " ameongeza rais wa Ufaransa.

Rais wa Ufaransa amesema hatishii nchi yoyote ya ukanda wa Sahel, lakini amebaini kwamba atachukua hatua ikiwa itahitajika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.