Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA-HAKI

Jacob Zuma kufuatiliwa kwa mashtaka ya rushwa

Mahakama Kuu ya Rufaa ya Bloemfontein, nchini Afrika Kusini imekataa rufaa ya rais wa nchi hiyo Jacob Zuma dhidi ya uamuzi wa kufuatiliwa kwa mashtaka 783 ya rushwa dhidi yake.

Jacob Zuma, tarehe 6 Agosti 2017 huko Pietermaritzburg, jimbo la KwaZulu-Natal.
Jacob Zuma, tarehe 6 Agosti 2017 huko Pietermaritzburg, jimbo la KwaZulu-Natal. © REUTERS/Rogan Ward
Matangazo ya kibiashara

Mchakato huo wa mahakama ulianza zaidi ya miaka kumi iliyopita wakati Jacob Zuma alikua bado hajakua rais wa nchi ya Afrika Kusini. Wakati huo, alishtakiwa kwa rushwa, udanganyifu na ukwepaji kodi. Mashtaka hayo yanayohusiana na mkataba mkubwa wa silaha uliyosainiwa mwaka 1999 na makampuni kadhaa, ikiwa ni pamoja na kampuni ya Ufaransa ya Thales. Lakini mashtaka yalifutwa na ofisi ya mashitaka kabla ya uchaguzi wa mwaka 2009.

Jacob Zuma na maafisa wengine wakuu serikalini walikuwa wametuhumiwa kupokea hongo wakati wa ununuzi wa ndege za kivita, maboti ya kushika doria na silaha nyingine.

Jumla ni Mashtaka 783 yanayohusiana na mkataba huo wa mwaka 1999 wa ununuzi wa silaha za mamilioni ya dola.

Mashtaka hayo yanahusiana na uhusiano kati ya Zuma na mfanyabiashara Shabir Shaik aliyepatikana na hatua mwaka 2005 ya kupokea rushwa kutoka kwa kampuni ya uuzani wa silaha ya Ufaransa "kwa niaba ya Zuma".

Ijumaa Mahakama ya Kuu ya Rufaa ya Bloemfontein ilithibitisha uamuzi wa mahakama wa mwezi Aprili mwaka 2016. Mahakama ya Pretoria iliamua kuwa uamuzi wa mwendesha mashtaka wa kufutilia mbali mashtaka dhidi ya Jacob Zuma mwaka 2009 " haukubaliki ". Rais na ofisi ya Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Jamhuri walikata rufaa na sasa wamepoteza kesi hii mpya.

Kwa sasa kazi kubwa iko mikononi mwa ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu, ambayo itabidi ianzeshe tena faili hii au la. Hali ambayo inaweza kupelekea kusikilizwa kwa kesi mpya. Jacob Zuma anaweza bado kuamua kwenda kwa Mahakama ya Katiba, Mahakama ya Juu zaidi nchini Afrika Kusini, lakini ana bahati ndogo ya kupwa nafasi hiyo.

Mashtaka hayo yaliwasilishwa mara ya kwanza dhidi ya Bw Zuma mwaka 2005 lakini yakaondolewa na waendesha mashtaka mwaka 2009 na kumuwezesha Bw Zuma kuwania urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.