Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-GUPTA-UCHUMI

Familia ya Gupta yaendelea na harakati zake Afrika Kusini

Familia ya Gupta, mshirika wa karibu wa Jacob Zuma, imetangaza kuuza makampuni kadhaa ya Afrika Kusini. Familia hii tajiri kutoka India inakabiliwa na shinikizo baada ya mfululizo wa ushahidi kuhusu ushiriki wake na utawala wa Jacob Zuma baada ya kuvuja kwa mamia ya barua pepe.

Waandamanaji wakibebelea picha ya mmoja wa ndugu wa familia ya Gupta Cape Town, Aprili 7, 2017
Waandamanaji wakibebelea picha ya mmoja wa ndugu wa familia ya Gupta Cape Town, Aprili 7, 2017 Wikimedia Commons / Discott
Matangazo ya kibiashara

Familia hii "Guptaleaks", imesem akuwa kwa sasa shughuli zake ziko hatarini. Benki kuu nne nchini zimefunga akaunti za Gupta miezi kadhaa iliyopita, na kuhatarisha shughuli za familia hiyo. Watu wanaonunua hisa za familia ya Gupta wanashtumiwa kufanya hivyo kwa kudanganya ili kuruhusu famili hiyo kuendelea na shughuli zake bila kuwa na wasiwasi.

Ni katika hali ya "kuokoa ajira" na "kusafisha jina lao ambalo limepakwa matope kinyume cha sheria na vyombo vya habari" ambapo familia ya Gupta imeamua kujitenga na vyombo vyake vya habari na shughuli zake za madini.

Inaarifiwa kuwa siku ya Jumatatu kituo cha televisheni cha ANN7 na gazeti la New Age, ambavyo vyote vinamilikiwa na familia ya Gupta, vilikua viliuzwa kwa mtu, asiyekuwa wa kawaida ambaye ni Mzwanele Manyi, msemaji wa zamani wa serikali anayejulikana kutoa msaada wake kwafamilia hii kutoaka India.

Itakumbukwa kwamba familia ya Gupta ndio ilitoa mkopo wa euro milioni 30 kwa ajili ya kununua vyombo hivyo vya habari, bila kujua vizuri jinsi gani Mzwanele Manyi atalipa mkopo huo.

Katika taarifa, kiongozi wa chama cha EFF (Fighters for Freedom Freedom), Julius Malema, amesema kuwa mpango huo ni "utani wa karne" na amelaani "shughuli za uhalifu".

Siku ya Jumatano, tuhuma ziliongezeka zaidi wakati familia ya Gupta ilitangaza kuuza kampuni yake ya madini ya Tegeta kwa Charles King SA, kampuni isiyojulikana kutoka Uswisi.

Siyo tu bei ya mauzo - iliyo chini ya euro milioni 200 - inaonekana kuwa ni kinyume kwa kampuni ya madini yenye ukubwa huo, lakini vyombo vya habari vya Afrika Kusini pia vimeonyesha kuwa mmiliki wa kampuni Charles King SA tayari amewahi kushirikiana na familia ya Gupta katika siku za nyuma.

Dalili nyingi zinaonyesha kwamba familia hii tajiri kutoka India bado inaendelea na shughuli zake Afrika Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.