Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-MAANDAMANO-USALAMA

COSATU yatoa wito kwa maandamno nchini Afrika Kusini

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini Afrika Kusini Cosatu pamoja na chama cha kikoministi wametoa wito wa mgomo wa kitaifa hivi leo kupinga kukithiri kwa rushwa nchini humo.

Kiongozi wa Cosatu Sdumo Dlamini akimshikilia mkono Jacob Zuma (katikati) wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa 10 wa Cosatu, Johannesburg, Septemba 21, 2009.
Kiongozi wa Cosatu Sdumo Dlamini akimshikilia mkono Jacob Zuma (katikati) wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa 10 wa Cosatu, Johannesburg, Septemba 21, 2009. AFPPHOTO/Paballo Thekiso
Matangazo ya kibiashara

Washirika hao wawili wa kihistoria wa chama tawala nchini Afrika Kusini cha ANC wanasema wamechoshwa na kukithiri kwa vitendo vya rushwa na uingiliaji katika udhibiti wa rasilimali za serikali, Lakini pia dhidi ya kupunguzwa kwa kazi, uongozi mbaya wa makampuni ya umma.

Hatua hii inaonyesha wazi mtengano wa washirika hao na chama tawala cha ANC ambacho licha ya kukabiliwa na matatizo chungu nzima bado kina idadi kubwa ya wawikilishi katika ngazi mbalimbali za uongozi.

Shirikisho hilo la vyama vya wafanyakazi pamoja na chama cha wa Kikoministi cha SACP wamekionya chama cha ANC kuhusu mpasuko uliopo baina yao na chama hicho.

Mashirika hayo yametowa wito mara kadhaa kwa rais Jacob Zuma kujiuzulu licha ya kwamba mtengano huo haaujatekelezwa.

Jumatano hii mashirika hayo mawili yamehamasiaha wafuasi wake katika miji 13 nchini humo kulaani wale wote wanaoiharibu nchi.

Licha ya kwamba sio maandamano ya kukipinga chama tawala au rais Jacob Zuma, chama cha wafanyakazi cha Numsa kilichofukuzwa katika shirikisho la Cosatu, pamoja na shirikisho mpya la wafanyakazi vimetowa wito kwa wafuasi wao kususia maandamano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.