Pata taarifa kuu
ZAMBIA-SIASA

Lungu aongoza uchaguzi Zambia huku upinzani ukisema kumekuwa na wizi wa kura

Raia wa Zambia wanaendelea kusubiri matokeo ya mwisho ya urais, baada ya kupiga kura wiki iliyopita kumchagua rais, wabunge na Mameya.

Kura zikihesabiwa nchini Zambia
Kura zikihesabiwa nchini Zambia dr
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Uchaguzi imetoa wito kwa raia wa nchi hiyo kuendelea kuwa watulivu na wavumilivu wakati huu ikiendelea kufanya kile kilicho ndani ya uwezo wake kutangaza matokeo yote.

Matokeo ya hivi karibuni yanaonesha kuwa rais Edgar Lungu anaongoza lakini ushindani ni mkali sana kati yake na mpinzani wake wa karibu Hakainde Hichilema.

Kati ya maeneo bunge 156 nchini humo, tayari matokeo ya maeneo bunge 132, yameshatangazwa na Lungu wa chama cha PF, anaongoza kwa kura 1,454,165, huku Hichilema wa chama cha UPND akiwa na kura 1,383,594.

Tofauti ya wagombe hawa ni kura 70,571.

Chama cha Hichilema kimetangaza kujiondoa kwenye kituo cha taifa cha kujumuishia matokeo jijini Lusaka, baada ya kudai kuwa Tume ya Uchaguzi ilikuwa imeshirikiana na chama tawala kuiba kura.

Huu ndio uchaguzi wenye ushindani mkubwa sana katika historia ya nchi hiyo ya Afrika ya Kati.

Ikiwa mshindi hatapata zaidi ya asilimia 50 na kura moja baada ya matokeo ya mwisho, basi kutakuwa na duru ya pili baada ya kipindi cha mwezi mmoja.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.