Pata taarifa kuu
ZAMBIA

Wananchi wa Zambia wanasubiri matokeo ya uchaguzi mkuu wa Agosti 11

Wananchi wa Zambia wanasubiri matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu ambao unatajwa kuwa ulikuwa wa ushindani mkubwa baina ya Rais Edgar Lungu na mpinzani wake wa karibu Hakainde Hichilema, anayemtuhumu kwa kushindwa kuimarisha uchumi wa taifa hilo. 

dr
Matangazo ya kibiashara

Rais Lungu ambaye alimshinda mpinzani wake kwa idadi ndogo ya kura katika uchaguzi wa mwaka jana, baada ya kifo cha mtangulizi wake Michael Sata, huenda akalazimika kuingia kwenye duru ya pili ya uchaguzi ikiwa hatapata nusu ya kura.

Licha ya kuwa matokeo rasmi ya awali bado hayajaanza kutolewa, maofisa wa tume ya uchaguzi wa Zambia, wanasema kuwa maelfu ya raia walijitokeza kushiriki kupiga kura kwenye uchaguzi wa Alhamisi, Agosti 11.

Uchumi wa taifa la pili kwa uzalishaji wa shaba, liko kwenye shinikizo kubwa kutokana na kupanda kwa gharama za usafirishaji wa madini hayo, huku Serikali ikijaribu kulishawishi shirika la fedha duniani IMF kuisaidia kifedha.

Wakati wa kampeni wafuasi wa chama tawala cha PF cha Rais Lungu walikabiliana mara kwa mara na wale wa kiongozi wa upinzani wa chama cha UPND, Hichilema, lakini hakukuripotiwa vutugu zozote wakati wa zoezi la upigaji kura.

Ikiwa matokeo hayatatoa mshindi aliyefikisha zaidi ya asilimia 50, badi huenda wagombea wawili waliopata alama za juu watachuana kweye duru ya pili ndani ya siku 37.

Hichilema ambaye ni mfanyabiashara na mtaalamu wa masuala ya uchumi, amesema yeye ndiye mgombea pekee anayefuzu zaidi ya Lungu kuongoza taifa taifa hilo.

Hata hivyo Rais Lungu mwenyewe anasema anahitaji muda zaidi wa kuwatumikia wananchi wa Zambia.

Tume ya uchaguzi ya Zambia yenyewe inasema itatangaza matokeo rasmi ya uchaguzi huu, Jumamosi jioni au mapema siku ya Jumapili mara baada ya zoezi la kuhesabu kura kukamilika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.