Pata taarifa kuu
ZAMBIA-SIASA

Mgombe wa upinzani nchini Zambia ashutumu tume ya uchaguzi na chama tawala kwa udanganyifu

Mpinzani wa rais katika uchaguzi wa Zambia, Hakainde Hichilema, ametoa madai ya kuwepo kwa udanganyifu katika uchaguzi huo jana Ijumaa, akishutumu maafisa wa uchaguzi na chama tawala kwa kula njama ya kuchelewesha matokeo katika mpambano huo mkali.

Kura zikihesabiwa nchini Zambia
Kura zikihesabiwa nchini Zambia dr
Matangazo ya kibiashara

Madai ya Hichilema yanatarajiwa kuweka mvutano zaidi kati ya wafuasi wa chama chake cha UPND na wale wa chama cha PF cha Rais Edgar Lungu

Zambia inafahamika kwa utulivu wake katika kubadilishana madaraka, lakini kampeni za uchaguzi ziligubikwa na juma moja la mapigano kati ya makundi hasimu, na kwa uchache watu watatu waliuawa katika kuelekea kwenye uchaguzi siku ya Alhamisi.

Hichilema amewaambia waandishi wa habari mjini Lusaka kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zambia ECZ kwa namna fulani inafanya hila kuchelewesha kutolewa kwa matokeo ili majambazi wa PF walio na silaha na bunduki wadhibiti vituo vya kupigia kura wakati wa usiku na kuandika matokeo feki, ambapo amesema wanajaribu kuzalisha matokeo.

Hichilema, mfanyabiashara tajiri ambaye anajaribu kwa mara ya tano kuwania urais, alikosa nafasi hiyo katika uchaguzi wa mwaka jana kwa tofauti ya kura 28,000 pekee dhidi ya rais Edger Lungu.

Mwaka huu, alidai kuwa kampeni zake zilikandamizwa na mamlaka kwa kupiga marufuku mikutano ya kampeni yake, kuwakamata viongozi wa chama na kunyimwa haki ya usawa katika kufikiwa na vyombo vya habari vya taifa.

Siku ya uchaguzi ambayo kulishuhudiwa wagombea tisa wakigombea urais, ilikuwa ya amani, na maofisa wa Zambia walirejea kutoa wito wa utulivu ili kujaribu kuzuia vitendo vya vurugu wakati wa matokeo.

Matokeo ya awali yalitarajiwa kutangazwa siku ya Ijumaa mchana, lakini yalicheleweshwa mara kadhaa mpaka yalipoanza kutolewa wakati wa jioni.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.