Pata taarifa kuu
DRC-BENI-USALAMA

DRC: Ishirini wauawa katika shambulizi jipya karibu na Beni

Watu zaidi ya ishirini waliuawa usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu wiki hii katika mji wa Apetina-Sana katika Wilaya ya Beni, katika Mkoa wa Kivu Kaskazini, siku chache baada ya mfululizo wa mauaji kutokea katika wilaya hiyo.

Askari wa FARDC akitoa ulinzi nje ya mji wa Oicha, wilayani Beni. (picha ya kumbukumbu)
Askari wa FARDC akitoa ulinzi nje ya mji wa Oicha, wilayani Beni. (picha ya kumbukumbu) © JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wilaya ya Beni, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaendelea kukumbwa na mauaji ya kikatili.

Haya ni mauaji ambayo yamezua wasiwasi kusababisha maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao.

Shambulio hilo la visu linadaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa kundi la waasi wa Uganda la ADF.

Shambulio ambalo lilitokea katika mji wa Apetina-Sana, kilomita 16 magharibi mwa Oicha, mji mkuu wa wilaya ya Beni, kwenye barabara kuu namba 4, sehemu ambayo wakaazi wa mji huo huita "pembetatu ya kifo", Mbau-Eringeti-Oicha.

Wawakilishi wa mashirika ya kiraia wamedai kuwa walionya, tangu Jumapili jioni, kuhusu kuwepo kwa watu wenye silaha na kushtumu, kwa mara nyingine, vikosi vya usalama kwa kuwa havikufanya chochote.

Akihojiwa na RFI, Mkuu wa Wilaya ya Beni, Donat Kasereka Kibwana, amebaini kwamba hata kama shambulio hili ni la kusikitisha, vikosi vya jeshi la DRC vinafanya kilio chini ya uwezo wao.

"Walikuja usiku kucha kuua watu, watu kumi na wanane. Tuliarifiwa asubuhi. Ni hali ya kusikitisha. Watu ambao walikuwa wamesalia katika eneo hilo wametoroka makaazi yao. Adui bado yuko Beni kwa muda mrefu. Anajua njia zote, njia zote za Beni na kwa hivyo, wakati askari wanajibu kwa mashambulizi adui anajua sehemu anakojificha. Ni hali ya huzuni na ya masikitiko, lakini wanajeshi wanafanya operesheni kubwa na adui yuko hatarini, " Kasereka Kibwana amesema.

Tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba na kuanza kwa oparesheni kubwa iliyozinduliwa na jeshi la DRC dhidi ya wanamgambo, mashambulizi dhidi ya raia yameongezeka na kupelekwa kwa jeshi la DRC katika eneo hakujazuia waasi kutekeleza mashambulizi mapya.

Kulingana na Teddy Kataliko, mkuu wa mashirika ya kiraia wilayani Beni, wanamgambo wa ADF wamebadilisha maeneo tangu kuanza kwa mashambuliziu ya jeshi.

"Adui aliyekuwa akiendesha maovu yake mashariki, sasa yuko katika eneo la magharibi ambapo raia wamekimbilia. ADF wanajaribu kukwamisha juhudi za majeshi, wakichukua raia kama ngao, " Teddy Kataliko amebaini.

Tangu Novemba 28, makao makuu ya jeshi la DRC yamehamia Beni ili kuwa karibu na uwanja wa mapigano. Katika eneo hilo, idadi ya vikoi vya jeshi imeongezeka karibu mara mbili, kutoka askari 11,000 hadi 21,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.