Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Hatma ya Omar al-Bashir kujulikana Jumamosi hii

media Rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir anashikiliwa mahabusu na anashtumiwa 'kumiliki katika njia haramu fedha za kigeni', 'kupata utajiri kwa njia haramu', kwa mujibu wa ofisi ya mwendesha mashtaka. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Mahakama kuu nchini Sudan, kesho inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu kesi ya tuhuma za rushwa inayomkabili rais wa zamani wa nchi hiyo Omar al- Bashir.

Kesi hii dhidi ya Bashir imekuwa ikisikilizwa mjini Khartoum tangu mwezi Agosti mwaka huu akituhumiwa kujipatia fedha kwa udanganyifu na matumizi mabaya ya fedha za wafadhili wakati akiwa rais.

Mnamo Juni 16, mwendesha mashtaka alisoma mashtaka dhidi ya rais huyo wa zamani, wakati alipoonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu kutimuliwa mamlakani na jeshi Aprili 11.

Tangu wakati huo Bashir anashikiliwa mahabusu na anashtumiwa "kumiliki katika njia haramu fedha za kigeni", "kupata utajiri kwa njia haramu", kwa mujibu wa ofisi ya mwendesha mashtaka.

Mwishoni mwa mwezi Aprili, mkuu wa Baraza la Kijeshi la Mpito, Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, alidai kwamba Dola sawa na zaidi ya milioni 113 taslimu zilikamatwa katika makazi ya Omar al-Bashir jijini Khartoum.

Alisema polisi, jeshi na maafisa wa usalama walipata Euro milioni saba, dola milioni 350,000 na Pauni za Sudani milioni tano (sawa na Euro milioni 93) wakati wa msako huo.

Bw Bashir aliingia madarakati kupitia mapinduzi ya kijeshi mnamo mwaka 1989, alitimuliwa na kukamatwa na jeshi Aprili 11 jijini Khartoum, chini ya shinikizo la maandamano ya kipekee yaliyozuka mwezi Desemba kufuatia kuongezwa mara dufu kwa bei ya mkate.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana