Pata taarifa kuu
UCHAGUZI NCHINI UGANDA

Wakimbizi kutoka DRC wahofia usalama wao

Nchini Uganda, siku chache kabla ya uchaguzi wa urais, uliopangwa kufanyika Januari 14, 202, wananchi wanaendelea kuwa na hofu ya kutokea kwa machafuko zaidi.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni GAEL GRILHOT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Yoweri Museveni anawania muhula wa sita akikabiliana na mpinzani wake mkuu,Bobi Wine, mwanamuziki nguli na maarufu nchini Uganda.

Kutokana na hali inayojiri kwa sasa nchini Uganda wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaoishi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala wameelezea wasiwasi wao juu ya kutokea kwa machafuko, hasa wanahofu kuwa waandamanaji wanaweza kuwashambulia.

Wengi wa wakimbizi hao tayari wameondoka katika mji wa Kampala na kujielekeza katika maeneo mengine ambayo wanaona ni salama

"Ninaogopa, ndio sababu nitaondoka Kampala kutokana na uchaguzi. Nitarudi kambini. Kwa sababu rais yupo, ndio sababu tuna amani hapa.

Wanasema, subiri tu, aondoke mamlakani, mtakiona cha mtima kuni, " amesema Inès mkimbizi kutoka DRC aliyekimbilia katika mji eneo la Nsambya huko Kampala. "Tunatukanwa, " ameongeza.

Wacongo wengi wanaoishi katika eneo la Nsambya wanahofia kulengwa na vurugu kuhusiana na uchaguzi huo.

Waganda wengi wanaona kuwa wakimbizi kutoka DRC wanamuunga mkono rais Yoweri Museveni, kwa mujibu wa Patience, mkimbizi mwingine kutoka DRC.

Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, zaidi ya wakimbizi 70,000 kutoka hasa nchini DRC, Sudan Kusini, na Burundi wanaishi katika mùji mkuu wa Uganda, Kampala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.