Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA-ICC-KABUGA-HAKI

Félicien Kabuga kukabidhiwa Mahakama Maalum ya Kimataifa ya IRMCT

Mahakama ya Rufaa jijini Paris nchini Ufaransa imeamua Félicien Kabuga, anayeshtumiwa kufadhili mauaji yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994, kutumwa katika Mahakama Maalum ya Kimataifa ya IRMCT.

Félicien Kabuga (picha ya kumbukumbu).
Félicien Kabuga (picha ya kumbukumbu). Nations Unies/AFP
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa majaji umejikita kuhusu uhalali wa waranti ya kukamatwa iliyotolewa na Mahakama Maalum ya Kimataifa ya IRMCT, mahakama ambayo ina majukumu ya kukamilisha kazi ya mahakama iliyokuwa inashughulikia kesi za Kimbari nchini Rwanda iliyokuwa mjini Arusha nchini Tanzania.

Bw. Kabuga anashtumiwa makosa saba, ikiwa ni pamoja na mauaji ya halaiki, uhalifu wa kivita; uhalifu dhidi ya binadamu na ufadhili makundi yaliyofanya mauaji ya kimbari mwaka 1994 nchini Rwanda, ambapo watu zaidi ya 800,000 (Watutsi na Wahutu wa msimamo wa Wastani) waliuawa na wanamgambo wa Iterahamwe kutoka chama tawala wakati huo cha MRND cha hayati rais Juvenal Habyarimana.

Hata hivyo wanasheria wake wamesema watakata rufaa katika kitengo cha mahakama ya juu nchini Ufaransa, wakibaini kwamba uamuzi wa kitengo cha Mahakama ya Rufaa ulikuwa wakisiasa.

Ikiwa wanasheria wa Kabuga watakata rufaa kesi hiyo huenda ikachukuwa muda nchini Ufaransa.

Félicien Kabuga alikuwa anataka ashtakiwe nchini Ufaransa.

Hivi karibuni Mahakama ya Rufaa ya jijini Paris nchini Ufaransa ilitupilia mbali ombi la kuachiliwa kwa dhamana kwa Félicien Kabuga.

Kwa mujibu wa taarifa ya mahakama ya Umoja wa Mataifa iIiyoanzishwa kwa ajili ya kuhumu kesi za uhalifu, IRMCT, Kabuga alihukumiwa mnamo mwaka 1997 kwa mokosa saba ya uhalifu ikiwa pamoja na ya mauaji ya halaiki, kuchochea mauaji na kushiriki katika mauaji.

Félicien Kabuga, alikuwa mtuhumiwa aliyewekwa kwenye mstari wa mbele. Kitita cha dola milioni tano kilitengwa kwa yeyote ambaye angetoa habari za kuwezesha kukamatwa kwake. Kwa muda wote huo alikuwa anatumia majina bandia.

Félicien Kabuga mwenye umri wa miaka 84, alikamatwa Jumamosi asubuhi Mei 16 nchini Ufaransa, nyumbani kwake huko Asnières sur Seine katika vitongoji vya Paris, nchini Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.