Pata taarifa kuu
TANZANIA-UFARANSA-USHIRIKIANO

Ufaransa Kushirikiana na Tanzania kufanya Utafiti katika Kilimo na Mazingira

Serikali ya Ufaransa imeingia makubaliano na serikali ya Tanzania kufanya mradi wa utafiti katika Mabadiliko ya Tabia nchi pamoja na kilimo endelevu kwa kushirikisha watafiti kutoka nchi hizo mbili, mradi utakaogharimu Dola laki nne.

Zao la mahindi ambalo limekuwa ni tegemeo kwenye mataifa mengi ya kusini mwa Afrika
Zao la mahindi ambalo limekuwa ni tegemeo kwenye mataifa mengi ya kusini mwa Afrika AFP/Patrick Hertzog
Matangazo ya kibiashara

Akizungumzia Hatua hiyo Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier amesema wamefikia hatua hiyo Baada ya taasisi ya utafiti barani Afrika IFRA pamoja na ile ya utafiti wa maendeleo endelevu IRD za kutoka nchini Ufaransa kujadiliana na serikali ya Tanzania na kukubaliana kufanya utafiti katika mabadiliko ya Tabia nchi pamoja na kilimo endelevu.

Akizungumzia namna Mradi huo Utakavyotekelezwa Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es salaam anayehusika na Utafiti alisema watashirikisha taasisi zinazohusika na utafiti ili kuwawezesha wataalam kupata ujuzi.

Mkurugenzi wa elimu ya juu kutoka wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania Prof.Adam Mwaikambo anasema uwekezaji hafifu unawaathiri watafiti,hali inayowalazimu kushirikiana na Ufaransa ili kufanikisha tafiti katika maeneo hayo ya kilimo na Mazingira

Katika Hatua nyingine,Serikali ya Ufaransa inafungua vituo vya Taarifa katika Chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM,Chuo Kikuu cha tafa Zanzibar SUZA pamoja na kituo cha utamaduni cha Alliance Francee ili kuwezesha wanafunzi wanaohitaji kusoma elimu ya juu ufaransa kupata taarifa, Dkt.Lulu Kaaya kutoka UDSM na Dkt Ali Makame Ausi kutoka SUZA wanasema ni fursa sasa kwa watanzania

02:18

STEVEN MUMBI WRAP Kuhusu UFARANSA-TANZANIA 09 OCT 2018 PAD

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.